HABARI KUBWA LEO,MGOMO MKUBWA BANDARINI,KUANZA HIVI KARIBUNI, TFFA WASEMA WAMECHOKA,SOMA HAPO KUJUA
Bandarini |
CHAMA cha
Mawakala wa Forodha Nchini (TFFA) kimeipa serikali wiki moja kupunguza dhamana
ya Tozo kwa mawakala wa forodha,lasivyo wataingia kwenye mgomo nchi nzima,ambao
mgomo huo utakahusisha Bandari zote
nchini,Mipaka pamoja na Viwanja wa Vya Ndege.Anaandika KAROLI VINSENT endelea
nayo.
Hatua hiyo imetangazwa leo Jijini Dar es
Salaam na Rais wa (TFFA) nchini Stephen
Katunga wakati wa mkutano na waandishi Habari ambapo amesema Tozo mpya ya
ushuru iliyopitishwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) –
kwa mawakala wa forodha kutakiwa kuweka Benki dhamana
ya milioni 100 ili kupata reseni ya kutoa uwakala wa forodha amedai kufanya
hivyo ni kurudisha Ubaguzi wa walichonacho na wasionacho.
Amesema Agizo hilo la TRA
linatawanyima uhuru katika soko la ushindani la Afrika mashariki ambapo amezidi
dai kuwa Amri hiyo haiko nchi nyingine yoyote huku akizingatia ina maana TRA
inawapenda sana wageni kuriko Watanzania.
Katunga amebainisha kuwa kwa njama ya TRA kwa kushirikiana na
makampuni makubwa pia kwa kutumia vibaya Mamlaka walizo nazo wameamua kuzifuta
kampuni za kitanzania ili kampuni kubwa na za kigeni wanaoitwa wawekezaji
waweze kufanya biashara hii.
Amesema TAFFA imejaribu kila aina ya njia kuwasiliana na Waziri wa Fedha nchini
Saad Mkuya lakini amekuwa amewapiga chenga na kukataa kuwasikiliza ndipo wote
kwa pamoja wamefikia hatua ya kuipa serikali wiki moja kuondoa tozo hiyo la
sivyo wakiakaidi watangaza mgomo nchini nzima
Hakuna maoni
Chapisha Maoni