Zinazobamba

ADC yaanza safari yake ya magogoni, mgombea wake achukua form muda huu NEC


Mgombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Alliance for democratic Change ADC CHIEF LUTASOLA YEMBA  muda huu amechukua Form yake ya kuwania urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania huku akisindikizwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho form zinazotolewa na tume ya Taifa ya uchaguzi.

Pichani ni mgombea huyo akiwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo Mgombea mwenza SAID MIRAJI,pamoja na mlezi wa chama hicho HAMAD RASHID.

CHIEF LUTASOLA YEMBA akizngumza na wanahabari mbalimbali waliojitokeza katika makao makuu ya Tume ya taifa ya uchaguzi kushugudia tukio hilo ambapo akiangumza na wahabarai hao amesema kuwa ni hakika kuwa sasa tanzania inahitaji kiongozi anayeweza kuyafikia matatizo halisi ya mtanzania na kiongiozi ambaye ana nia ya dhati ya kuwasaidia watanzania jambo ambalo amesema kuwa kama watanzania watamwamini na kumpa nafasi ya kuiongoza Tanzania atahakikisha kuwa atawatumikia watanzania kwa uwezo wake wote

SAID MIRAJ ni mgombea mweza wa nafasi ya urais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ambapo akizngumza na wanahabari amesema nchini tanzania sasa upinzani wa kweli haupo kilichobali ni kuwatania watanzania hivyo chama cha ADC kimekuja kuwakomboa watanzania na kuleta upinzani wa kweli katika siasa za tanzania 

HAMAD RASHID ni mgombea wa Urais wa Chama hicho kwa upande wa Zanzibar ambapo leo pia alikuwa mmoja kati ya viongozi waliomsindikiza mgombea huyo katika nkuchukua Form ya kuwania Urais.

Hakuna maoni