Zinazobamba

WALIOMUUA KIGOGO WA POLISI WAKAMATWA,KAMANDA SIRRO ASEMA YAKE,SOMA HAPO KUJUA

 Kamishna wa Polisi, Simon Sirro

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya dare s Salaam limewakata watu watatu waliohusika na tukio la mauaji ya Afisa wa polisi A.S.P Elibariki Palangyo lilotokea siku ya tahehe 4 mwezi huu nyumbani  kwake yomba wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
       Akithibitisha kuwakamata watu hao,Naibu Kamishna wa Kanda maalum ya Polisi Mkoani Dar es salaam Samwel Sirro leo Jijini dare s Salaam wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema baada ya tukio hilo kutokea jeshi lake kwa kushikirioana na jeshi la Polisi wilayani Temeke lilifanya msako mkali na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao watatu wanaosadikiwa kuhusika na mauajia hayo.
         Sirro amewataja watuhumiwa hao ni Salim Ktahib,Miaka 32 ambaye ni Dreva wa Bodaboda mkazi wa Tabata luis jijijni Hapa ambaye alikamatwa maeneo ya Kiwalani akiwa mafichoni.
        Mwengine Ismail Said miaka 36 naye pia ni Dereva bodaboda na Mkazi wa Yombo Makangarawe .
           Sanjari hao pia Kamanda Sirro alimtaja mwengine ni Pirimini Haulemi,miaka 25 makazi wa Yombo Mkangarawe naye pia ni dreva Boda boada.
           Aidha,Kamanda Sirro amesema Jeshi hilo bado linaendelea na msako mkali ili kuweza kuwabaini watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo,
          Wakati huo huo pia Jeshi hilo limewaka watu watano wakiwa na sare za Jeshi la Wananchi wa Tanzania kinyume na sheria.
         Ambapo inadaiwa watu hao  walikamatwa siku ya tarehe 5 mwaka huu maeneo ya Tandika Manispaa ya Temeke na skari wa doria.

           Vilevele paia Jeshi hilo limewakatama watu watutu wakiwa wamekutwa na nyara za serikali aina ya Meno ya temba ambao nao pia waliakamtwa maeno ya Tandale.

Hakuna maoni