UKAWA, CCM WAKIMBIA KIKAO CHA WANAHARAKATI WA MJUMITA
Ni kama wamekimbia, vyama vya siasa vikiongozwa na chama tawala pamoja na ukawa wamekimbia kikao cha pamoja na wanaharakiti kilichokuwa na lengo la kujadili mustakabali wa kulinda misitu kwa uhai wa wananchi.
Akizungumza kwa mwandishi wa Mtandao huu mapema hivi karibuni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi amesema wanasiasa hao wamekacha kikao hicho licha ya kuahidi kufika hadi dakika za mwisho
Njahidi alisema lengo la kuwakutanisha wanasiasa hao katika kikao chao ni kutaka kuwaambia umuhimu wa kuhifadhi mazingira na ikiwezekana waeleze ni jinsi gani ajenda zao za chama zimedhamiria kulinda misitu.
Alisema lakini kwa bahati mbaya, wamekimbia kikao hicho hatua inayowafanya kubadili mbinu ya kufikisha ujumbe ilimisitu iweze kudumu kwa faida ya vizazi na vizazi.
Akizungumzia umuhimu wa wanasiasa kuambiwa ukweli juu ya kulinda misitu, Njaidi alisema wanasiasa wanachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu misitu wakati wanapoomba kura kwa kuruhusu wananchi wao kuvamia misitu.
Alisema mfano mzuri ni wa waziri Njarandu ambaye aliruhusu wananchi wake kuvamia msitu na kuharibu kabisa vyanzo vya maji. hata hivyo wamesema wanajipanga kuja na mbinu mpya ya kufikisha ujumbe.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (Mjumita), Rahima Njaidi akiendelea kuzungumza ambapo MJUMITA inawataka wagombea wa ngazi mbalimbali katika uchaguzi huuo pamoja na mambo mengine kuzungumzia juu ya uhifadhi wa mazingira katika mikutano yao hasa kutokana na umuhimu wa mazingira katika ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
"Kukemea wanasiasa na viongozi wengine watakaotoa kauli zitakazokinzana na sera na sheria za misitu.
MJUMITA imesema Kumekuwa na desturi ya baadhi ya wanasiasa kutoa kauli zinazokinzana na sheria na sera za misitu. Baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakitoa matamko na ahadi (hasa wakati wa uchaguzi) kwamba kwa nafasi zao watashawishi shughuli za kibinadamu kuruhusiwa katika maeneo ya hifadhi za misitu.
"Kauli za namna hiyo zimekuwa na athari kubwa kwenye juhudi za uhifadhi wa misitu nchini ikiwa ni pamoja na baadhi ya misitu kuvamiwa na wananchi. Wanamtandao tunataka serikali na viongozi watakaochaguliwa,".....:
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA),Rehema Ngelengele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA),Rehema Ngelengele akizungumza. Kulia ni Kiongozi Mtetezi wa Jamii waishio kandokando ya Misitu (CAL), Revocatus Njau.
Wajumbe wakifuatilia.
Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu nchini (MJUMITA),Rehema Ngelengele (kulia) na Mkurugenzi wa Mjumita, Rahima Njaidi wakifuatilia mada wakati wa uwasilishaji wa Mazimio hayo.
Wajumbe na washiriki wakifuatilia mada katika mkutano huo.
Elias Monga, Meneja mradi akiwasilisha maazimio hayo ya wananchi kwa wajumbe wa Bodi ya Mjumita.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni