HABARI ILIYOTIKISA JIJI-KUJIUZULU KWA LIPUMBA,TAARIFA KAMILI HII HAPA,NI HUZUNI CUF,BOFYA HAPO KUJUA
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Peacock leo jijini Dar es salaam wakati akitangaza kujuuzulu nyazifa zake zote katika chama hicho na kubaki mwanachama wa kawaida kutokana kile alichokiita dhamira inamsuta. |
MWENYEKITI
wa Chama cha Wananchi CUF Profesa ibrahimu Lipumba ametangaza Rasmi kujiuzulu
nafasi ya hiyo ya uenyekiti na kusema atabaki kuwa mwananchama wa Kawaida wa
chama hicho.Anaadika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Akitangaza uamuzi huo leo Jijini Dar
es Salaam wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema amefikia
hatua hiyo huo baada ya “kutorizishwa” na hatua ya Umoja wa Vyama vya Upinzani
Vinavyounda Ukawa kumchukua waziri mkuu wa Zamani Edward lowassa kutoka Chama cha Mapinduzi CCM na kumpatia
nafasi ya kupeperusha Urais kuperusha bendela ya Umoja huo kwenye uchaguzi
mkuu wa hapo baadae.
Prof Lipumba amesema hawezi
kukubali kumuunga mkono Lowassa kwa kile anachodai kuhusika katika kupitisha Katiba iliyopendekezwa na
Bunge maalum ambayo anadai imekiuka misingi ya haki ya Binadamu.
Amesema hata Umoja wa Ukawa ambao ni
Munganiko wa Vyama vya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema,NCCR-mageuzi
pamoja na NLD anadai muunganiko huo ulitokana na kupinga Mwenendo wa lilokuwa
Bunge Maalum la Katiba, ambapo sasa anashangaa leo viongozi wenzake wa Ukawa kulisahau hilo na kumuunga
mkono Lowassa ambaye adai alihusikika kwa kiasi kikubwa katika kupitisha Katiba
pendekezwa.
Mwanasiasa huyo msomi wa masuala ya Uchumi
amesema hakurupuka kufikia uamuzi wake ,kwani ametafakari kwa makini na ameamua
kumwandikia barua katibu mkuu wa chama cha CUF ya kutaka kujizulu na kutaka kubakia
kuwa mwanachama wa kwaida.
Amesema hawezi kuhama CUF kutokana
na yeye kukipigania kwa kipindi kirefu ikiwemo kukitamburisha kwa
wananchi,ambapo amedai kupigwa hata kufunguliwa kesi ya mahakamani yote hayo kwa
ajili ya kukijenga chama hicho.
Ameongeza kuwa ataendelea kukishauri
chama chake kwenye masuala ya kiuchumi na kisiasa.
Waandishi wa Habari wakamuuliza, je
kujiuzulu kwake huko kwenye dakika za mwisho kabla ya uchaguzi mkuu kuanza je
uwenda umetokana na madai yanayotambaa
kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuhongwa
pesa na CCM ili auvuruge ukawa-,
Ndipo akasema hata angekabi kuwa mwenyekiti wa CUF pia hata
madai ya yeye kuhongwa na Lowassa ili wamkaribishe UKAWA yangethibitika kuwa ni
ya kweli.
WADAU WA WANENA,
Wanadau mbali mbali wamezungumiza
hatua hiyo,Akiwemo Mwandishi wa Habari mzoefu wa Redio One Cristofa James
amesama kitendo alichofanya Lipumba cha kujiuzulu dakika za mwisho kinazidi
ibua mashaka.
“Watanzania wanatakiwa kuwapima
wanasiasa kweli kweli kipindi hiki,hapa hakuna jipya huyu Lipumba katika mkutano wake na waandishi
wa habari akiwepo na wenzake alisema wanamkaribisha lowassa aje kujiunga na
Ukawa,leo amekuja anajizulu,inakuwaje sasa mtu huyu abadirike na kusema kwamba
hamtaki lowassa,je huyo si atakuwa amenunuliwa hapo”
UTATA WAGUBIKA CUF.
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida
utata umegubika ndani ya Chama cha CUF baada wanachama na viongozi kutoamini
hatua aliyofikia ya Kutojiuzulu.
Utata ulianza pale ambapo taarifa za
Prof.lipumba kuzungumza na waandishi wa Habari,baada ya taarifa ya kuwepo na
mkutano na waandishi wa Habari kwenye chama hicho huwaga inatolewa na Afisa Uhusiano wa chama hicho
Bwana sailas ambapo leo waandishi wa habari aliposikia taarifa hiyo walimuuliza
Afisa habari huyo akisema chama cha CUF hakina mkutano na waandishi wa habari.
Baada ya taarifa hiyo,waandishi
hawakuchokua kufuatilia ndipo wakabaini mkutano wa Lipumba unafanyika katika
Hoteli moja hapa Jijini.
Profesa Lipumba alifika hotelini hapo
akiwa na Gari la chama hicho,huku likiwa limetolewa bendela ya CUF .
Ndipo Profesa huyo akashuka kwenye
Gari hilo akiwa na hana Mlinzi wa chama hicho huku akiongozana na Dereva wa
gari lake tu kinyume na kawaida ambapo alikuwa anaongoza na Naibu Katibu mkuu
wa CUF bara Magdalena Sakaya.
ENDELEA KUFUATILI FULLHABARI.BLOGS utapata
mkasa mzima.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni