MFUMUKO WA BEI JUUU-OFISI YA TAKWIMU YASEMA HALI BADO NI TETE,SOMA HAPO KUJUA
Pichani ni Mkurugenzi wa wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo |
MFUMUKO wa Bei nchini umeongezeka katika kipindi cha mwezi Julai hadi kufikia asilimia 6.4 toka asilimia 6.1 kwa
mwezi Juni mwaka huu,Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa wa Sensa za Jamii na Takwimu za Uchumi wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu, Ephrahim Kwesigabo wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo
amesema
kuongezeka huko kwa mfumuko wa bei kumetokana na kasi ya upandaji wa bei za
bidhaa na huduma kwa mwaka ulioshia
mwezi julai 2015,
Kwesigabo amesema
Fahirisi za bei zimeongezeka kwa hadi
158.78 kwa mwezi huo wa Julai
kutoka kwa 149.16 mwezi huo huo wa julai wa mwaka 2014.
Amesema hata bei ya Bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi
Julai 2015 ,umeongezeka hadi hadi kufikia asilimia 10.6 toka asilimia 10.1 kwa
mwezi juni 2015.
Aidha,kwesigapo amesema mfumuko wa
bei katika nchi za afrika mashariki bado Tanzania mfumuko wake unazidi kuwa
mkubwa ukilinganisha na Kenya, na Uganda.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni