Zinazobamba

MAUZO YA SOKO LA HISA DSE YASHUKA,SOMA HAPO KUJUA

Meneja Mradi na biashara wa soko la hisa hapa nchini, Patrick Msusa akizungumza na na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,picha ya Matkaba

SOKO la Hisa Mkoani Dar Es Salaam (DSE) limesema mauzo ya hisa yameboromoka kufikia asilia 41.80 tofauti na wiki iliyopita.Anaandika KAROLI VINSENT endelea nayo.
  Akitangaza hali hiyo leo Jijini Dar Es Salaam, Meneja Mradi wa Biashara wa (DSE) bwana Patrick Msusa Wakati wa Mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema mauzo ndani ya soko hili yameboromoka toka mauzo ya Bilioni 2.5 ya wiki iliyoita hadi kufikia bilioni 1 ambayo ni sawa na asilimia 41.80.
         Msusa amezitaja sababu ya kushuka kwa mauzo ni yametokana na wawekezaji nchini kushindwa kuziuza hisa zao wanazo zinunua katika soko hilo,sanjari na kuishuka kwa Thamani ya shiilingi Tanzania.

          Pamoja na hayo pia Soko hisa limesema licha ya kushuka kwa mauzo hayo lakini bado bado benk ya CRDB imeendelea kuwa kinara wa mauzo ya hisa zake akifuatia na Benk ya NMB.

Hakuna maoni