Zinazobamba

GHARIKA LA LOWASSA KUTUA ARUSHA KESHO,MJI KUFUNGWA KWA SAA TANO,SOMA HAPO KUJUA


Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha kupitia chama cha CUF Salussingo Omari
 akizungumza na vyombo vya habari.


Waziri mkuu mstaafu Edward  Lowassa ambaye ni mgombea Urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)anatarajiwa kupokelewa kwa mapokezi makubwa ikiwemomagari,pikipiki,katika uwanja wa ndege wa  kia hadi viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe  15) ambapo atahutubia wananchi katika mkutano ulioandaliwa na chama 
hicho.
       Akizungumza mapema jana na  waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho juu ya maandalizi hayo  Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa alisema kuwa mapokezi hayo yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukiohilo ni la kihistoria 

Mwenyekiti wa chadema Mkoa wa Arusha Amani Golugwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya mapokezi ya mgombea Urais  Edward Lowassa kupitia  CHADEMA  yamekamilika kwa asilimia miamoja na tukio hilo kuliita la kiistoria ambalo litafanyika katika viwanja vya tindigani kata ya kimandolu jijini Arusha siku ya jumamosi(kesho tarehe 15)(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

         Alisema kuwa  lengo  la ujio huo ni kumtambulisha mgombea urais ambaye ataambatana na mgombea mwenza Juma Duni Hajji ,kwa kuwatambulisha kwa wananchi wa Mkoa wa 
Arusha sambamba na kupata udhamini wa wananchama waliojiandikisha kupiga
kura

            Pia alisema kuwa zoezi la udhamini umeshaanza Arusha na  uongozi wa Tume umaelekeza mgombea kupata wadhamini 300 na  jimbo la Moshi mjini wataoa wadhamini 300

      Aidha aliwataka ,wakazi wa jijili la Arusha na waliopo jirani kujitokeza kwa wingi katika tukiohilo
la kihistoria ambapo pia viongozi wakuu wa chama hicho watahudhuria  akiwemo Mwenyekiti wa Taifa Freeman Mbowe,wenyeviti wenza wa ukawa 
kutoka NLD,NCCR pamoja na chama cha CUF,John Mnyika ,Nibu katibu mkuuZanzibar Salum Mwalimu na viongozi wengine wengi.


          “Kwakushirikiana na jeshi la polisi pamoja na vikosi vyetu suala la Amani,Utulivu,Ulinzi na Usalama 
vitadumishwa katika msafara huo pamoja na mkutano huo”Alisema Golugwa

          Hata hivyo baada ya mkutano huo kuisha msafara huo utaelekea katika jimbo la Monduli ambapo pia  Mh.Lowassa atapata wasaa wa kuhutubia wananchi katika jimbo hilo
          Kwa upande wake Naibu katibu  mkuu waTimu Lowassa for president  Ndama Jeuri alisema wamejiandaa  vizuri kumpokea  na wataendelea kuhamasisha watu kumuunga mkono Lowassa 
katika harakati zake za Urais

Katika msafara huo zaidi ya magari 75 yataanzia katika ofisi za chadema hadi katika uwanja 
wa ndege wa kia huku vikundi mbalimbali vya ngoma vikitumbuiza wakati wa
mapokezi ya Lowassa.

Hakuna maoni