Zinazobamba

WATOTO WA TANZANIA WAKO HATARINI KUPATA MTINDIO WA UBONGO-TFNC

Afisa Lishe JULIETH SHINE akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu afya na lishe ya mama mjamzito na anayenyonyesha . Afisa huyo amesema ni haki ya mtoto kupata lishe bora na  kunyonyeshwa kwa wakati vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya. tafiti zinaonyesha kunyonyesha kunapunguza vifo vya watoto kwa asilimia 13.
aKIFAFANUA ZAIDI.

Wanahabari wakifuatilia kwa makini semina hiyo ya siku moja, katika semina hiyo wataalamu wamefafanua juu ya dhana ya kubemenda wakisema mzazi anaweza kukutana na mme wake baada ya siku 42 na hakuna tatizo lolote linaloweza kutokea. kikubwa kunahitajika usafi wa hali ya juu na mapenzi kwa mtoto. 
Na Karoli Visenti.
Imeelezwa kuwa watoto chini ya umri wa miaka miwili wapo hatarini kupata mtindio wa ubongo kutokana na wazazi kujikita zaidi na kazi wakisahau kuwanyonyesha ipasavyo wsatoto wao.

Akizungumza katika semina maalum kwa wanahabari mapema hii leo Jijini Dar es Salaam,wataalamu kutoka Taasisi ya chakula na lishe Tanzania wamethibitishwa hali hiyo kutokea kama hatua za haraka hazitachgukuliwa na wamama wajawazito na wanaonyonyesha.
        Afisa lishe Neema Joshua ameuambia mtandao huu katika mahojiano maalum kuwa hali ni mbaya na kuna haja ya watanzania kuunganisha nguvu kupigania watoto kupata haki yao ya msingi ya kunyonya ili tuwe na taifa lenye watu wazuri.
         Amesema hali ilivyo watu wamejikita zaidi kupenda kazi kuliko kuangalia watoto wao jambo linalotia shaka kwa watoto hao kuwa na afya njema.

Hakuna maoni