Zinazobamba

UKAWA WATAJA VIGEZO VYA UDIWANI,SOMA HAPO KUJUA

Naibu Katibu Mkuu CUF, Magdalena Sakaya
Naibu Katibu Mkuu CUF, Magdalena Sakaya

MAKATIBU wakuu wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), jana walisaini makubaliano ya utaratibu wa kufuatwa katika kusimamisha mwakilishi mmoja katika ngazi ya udiwanianaandika Faki Sosi … (endelea).
        Mkutano huo uliohusisha makatibu wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), NCCR-Mageuzi, Chama cha Wananchi (CUF) na National League for Democracy (NLD) ulifanyika ukumbi wa makao makuu ya Chadema, Kinondoni, Dar es Salaam.
            Makubaliano hayo yalitangazwa katika mkutano uliohudhuriwa na Kaimu Katibu Mkuu NCCR-Mageuzi, Dk. George Kahangwa, Naibu Mkuu CHADEMA, John Mnyika, Katibu Mkuu NLD, Tozzy Matwanga na Naibu Katibu Mkuu CUF, Magdalena Sakaya.
          Sakaya akisoma taarifa ya muafaka uliofikiwa, alitaja vigezo vya kuzingatiwa katika kusimamisha mgombea mmoja atayewakilisha vyama hivyo. Vigezo hivyo ni (i) Matokeo ya Uchaguzi 2010, chama kinachotawala katika Kata husika, idadi ya kura ambazo chama mshirika wa UKAWA endapo hata hiyo Kata hiyo ipo chini ya CCM, matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2014, mtandao wa chama katika Kata husika, mila, desturi na utamaduni wa jimbo au kata husika, na mgombea anayekubalika katika jamii.
               Amesema vyama vya UKAWA vitatumia njia ya ushirikiano na maridhiano ya chama gani kiachiwe kugombea Kata. Pia suala la kuzingatia kupata mgombea asiyekuwa na kashfa na anayekubalika katika jamii linapaswa kuchukuliwa kwa umuhimu mkubwa.
  Habari hii kwa hisani ya Mwanahalisi oline

Hakuna maoni