GAZETI LA UHURU LAUMBULIWA,SERIKALI YAMSIFU LOWASSA,SOMA HAPO KUJUA
NA KAROLI VINSENT
SIKU chache kupita baada ya Gazeti linalotumika na chama cha
Mapinduzi CCM kueneza sera za kiplopaganda la Uhuru kudai vibaka walitawala wenye Maandamano ya kumsindikiza mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua
fomu juzi.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias
Chikawe Amelishukia gazeti hilo na kusema wao kama serikali wamefurahishwa na
amani iliyotawala wakati wa maandamano hayo.
Waziri Chikawe ameitoa
kauli hiyo leo wakati alipokuwa anazungumza na kituo kimoja redio nchini, ambapo amesema
alishuhudia umati mkubwa wa watu
wakiimba na kucheza katika hali ya amani na hilo ni jambo zuri linalopasa
kuendelea wakati wote.
Amesema anatarajia hali hiyo itaendelea hata mikoani mgombea
huyo akienda.
“Tumefurahi, kulikuwa na amani ya kutosha, watu walikuwa wengi zaidi
ya ilivyokuwa kwa CCM,” amesema Waziri Chikawe.
Aida,Waziri Chikawe alikiri maandamano hayo kusimamisha shughuli
katika baadhi ya maeneo ikiwamo ofisi yake ambayo haikupokea wageni kwa saa
kadhaa.
Wakati huohuo,
Chikawe alionya: “Tunaomba wanasiasa na mashabiki wao wasitembee na silaha
kwenye mikutano yao, waziache mahali salama nyumbani na pia wawaache polisi
wafanye kazi yao ya kuwalinda wote.”
Waziri Chikawe alisema mabomu ya machozi yanayotumika kazi yake
siyo kuua au kuumiza watu bali kuzuia wasifanye vurugu.
Hata hivyo, Waziri Chikawe alisisistiza ushiriki wa viongozi wa
vyama vya siasa ni muhimu katika kufanikisha hilo.
Alisema wanasiasa wanapaswa kujiheshimu kwa kukwepa kampeni za
uchochezi na kauli zinazoweza kusababisha fujo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni