Zinazobamba

SERIKALI YA WATU WA CHINA YAGUSWA NA UJANGILI WA TEMBO NCHINI,YAZINDUA KAMPENI KUMALIZA TATIZO HILO,SOMA HAPO KUJUA


Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (katikati), akihutubia wakati akizindua kampeni ya kupambana na ujangili viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam leo asubuhi. Kampeni hiyo imeanzishwa na watu wa China kwa ajili ya kuunga jitihada za watanzania katika mapambano hayo ya kuwalinda wanyama dhidi ya ujangili hasa tembo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira kwa niaba ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kinondoni, Faudhia Eddy katika uzinduzi huo. Balozi huyo alitoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing (kulia), akimpa zawadi ya mpira, Mwalimu Flora Lukali kutoka Shule ya Mount Pleasant kwa ajili ya shule hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania, Dk.Lu Youqing akionyesha umahiri wa kuchezea mpira katika uzinduzi huo kabla ya kutoa zawadi ya mipira kwa baadhi ya shule za Manispaa ya Kinondoni.
Wanafunzi wakiwa na vipeperushi vya bendera ya nchi ya china wakati wa uzinduzi huo.
Wasanii wa kundi la makhirikhiri wakitoa burudani katika 
uzinduzi huo.
Wanafunzi wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wimbo wa taifa ukiimbwa.
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.
Wanafunzi ndani ya uzinduzi huo. 

Suleiman Msuya

WATANZANIA hasa vijana wametakiwa kuwalinda wanyamapori ili wawe kichochoe cha uchumi wa nchi na wananchi.

Hayo yalisemwa Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing, Dar es Salaam leo asubuhi viwanja vya Leaders wakati akizindua kampeni za kupiga vita ujangili, kwa waendesha baskeli kuendesha kutoka Dar es Salaam hadi Arusha.

Dk. Youqing alisema wanyamapori ni rasilimali muhimu katika kukuza uchumi na maendeleo hivyo juhudi za kupambana na ujangili zinahitaji kuongezeka kwa faida ya sasa na miaka ijayo na vijana ndio wenye wajibu mkubwa.

Alisema iwapo kila Mtanzania hasa kijana atashiriki katika mapambano hayo ni dhahiri ujangili ambao unaonekana kushika kasi utapungua ua kuisha kabisa.

"Wanyamapori ni kichochoe cha utalii ambao unaingizia Taifa fedha hivyo kukuza uchumi wa nchi na wananchi, hivyo China kwa kushirikiana na wadau mbalimbali tumeamua kusaidia kampeni hii ya uendesha baskeni ili kupiga vita hii," alisema.

Alisema kampeni hiyo inatarajia kujengea uelewa wananchi kuacha ujangili hasa wa Tembo ambao wamekuwa wakikutana na changamoto ya kuwindwa kila mara.

Balozi Youqing alisema katika mapambano ya kuzuia ujangili ubalozi wao umetoa sh. bilioni 2.6 ili kusaidia ununuzi wa vifaa mbalimbali vya kupambana na hali hiyo.

Kwa upande wake Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini wa taasisi ya Authorized Association Conceptive (AAC), Mohammed Kamuna, alisema watashirikiana na ubalozi wa China katika mapambano hayo.

Kamuna alisema kupitia ushirikiano huo anaamini kuwa kuna faida itapatikana  moja kwa moja kwani jamii itapata uelewa kuhusu madhara ya ujangili kwa wanyamapori hasa tembo.

Hakuna maoni