Zinazobamba

UPINZANI KUONGOZA NCHI HII NI SAWA NA MBOWE KUONYESHA CHETI CHAKE CHA FORM SIX KWA WAANDISHI WA HABARI.



Na Thadei Ole Mushi
Ni kwa wenye akili kubwa ambao akili zao ni zaidi ya GB 1000 ndio wanaoweza kukubaliana na mm tu, hawa ambao akili zao zinasoma kwenye MB bado tuwaache kwenye vijiwe vya bangi na viroba wakisubiri Lowasa aingie IKULU.
Nasema hivi kwani takwimu zinanipa authority ya kufanya hivyo. Nimekuwa nikifuatilia siasa za nchi yangu toka enzi za kuchagua mtu na kivuli mimi sikuletwa kwenye siasa na yale mafuriko ya Mrema 1995 wala haya ya Mtafuta Ikulu Edo . Amini usiamini kuitoa CCM madarakani inahitaji zaidi ya karne mbili zijazo ila kwa namna ya upinzani tulio nao sahau kabisa jambo hilo kwa sasa.
Kama na wewe ni muumini wa QUNTITATIVE ANALYSIS utakubalina na hiki ninachokisema hebu tuangalie data zinatuambia nini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania 1992.
Baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nchini taifa kwa mara ya kwanza lilikwenda kwenye uchaguzi 1995 uchaguzi ambao ulishirikisha vyama vingi vya siasa. Upinzani ulionekana mkubwa kwa watu wawili MKAPA na MREMA japokuwa vyama vingine pia vilikuwepo. Katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 1995 Mgombea wa CCM Benjamin Mkapa alipata kura 4,026,422 wakati mgombea wa NCCR-Mageuzi Bw. Augustine Lyatonga Mrema alipata kura 1,808,616. Wapiga kura walikuwa ni 6,846,681. HIvyo, Mkapa alipata asilimia 61.82 wakati Mrema akipata asilimia 27.77
Baada ya uchaguzi huo Raisi mkapa aliingia madarakani na kuitoa Tanzania kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kwa kifupi ni kwamba mkapa alifanya mambo makubwa sana katika kipindi chake cha kwanza jambo lililowapa wananchi imani kubwa sana juu yake na kumrudisha kipindi cha pili kwa ushindi mkubwa zaidi ukilinganishwa na ule wa mwaka 1995. Hakuna haja ya kuorodhesha mambo aliyoyafanya mkapa hapa kwani kila mtu anayajua.Uchaguzi wa Mwaka 2000 CCM ilifanya vizuri zaidi kuliko miaka mitano nyuma. Rais Mkapa alipata asilimia 71.74 ya kura zote za Urais 5,863,201 wakati Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF akipata asilimia 16.26 ya kura za Urais 1,329,077 wakati Augustine Mrema akigombea mara ya pili akipata kura 637,077. Wapiga kura waliojiandikisha wakiwa 10,088,484 na waliopiga kura wakiwa 8,517,598 sawa na asilimia 84.4.Katika chaguzi zote hizi mbili CHADEMA hakikuwahi hata kushika number tatu wakati number moja imekuwa ikishikwa na ccm huku number mbili na tatu vyama vya CUF na NCCR vikibadilishana nafasi.
Mwaka 2005 CCM ikiwa imebadilisha mgombea kama katiba ya chama chake inavyosema iliendelea kungara huku vyama vingine vingi vikiendela kusimamisha wagombea wale wale waliendelea kuwa wapambe wa bwana harus CCM Kana ilivyo kawaida mpambe kazi yake ni kumsindikiza bwana harusi kila mahali ila ikifika muda wa kulala huwa nje ya kuta nne za chmba cha bwana harusi ndivyo hivyo kwa wapinzani walikuwa wakiishia kwenye sherehe za kuapishwa pale uwanja wa uhuru. Katika uchaguzi huu wa mwaka 2005 bendera ya ccm ikipeperushwa na Jakaya Mrisho Kikwete mgombea wa ccm alipata kura 9,123,952 sawa na asilimia 80.28 wakati mgombea wa upinzani Prof. Lipumba akipata kura 1,327,125 wakati Freeman Mbowe akipata kura 668, 756 sawa na asilimia 5.88.Kwa mara ya kwanza CHADEMA ikijitokeza kwenye 3 bora huku wakiambulia kura 668, 756 sawa na asilimia 5.88 sawa na idadi ya wakazi wa wilaya moja kwa baadhi ya wilaya za Tanzania.
Mwaka 2010 Rais Kikwete alipata kura 5,276,827 sawa na asilimia 62.83 wakati Dr. Slaa mgombea wa CHADEMA akipata kura 2,271,941 sawa na asilimia 27.05 ya kura za Rais huku Prof. Lipumba akipata asilimia 8.28 ya kura za Rais. Kutoka kura 9,123,952 alizopata mwaka 2005 hadi kura 5,276,827 ni anguko kubwa kwani alipoteza angalau kura milioni 3,847,125. Katika uchaguzi huu ile mamluki ya NCCR ikawa imehamia chadema na kukifanya kushika nafasi ya pili. Hapa kwa mwana ccm yoyote atakubaliana na mm kuwa asilimia za ushindi kwa vipindi vyote ilishuka zaidi ila kuna sababu zake mojawapo ya sababu hizo ni:-
1. Baada ya kipindi cha kwanza cha uongozi wa JK wananchi walikuwa wanatarajia kasi zaidi ya maendeleo kuizidi ile ya Mkapa ila hawakujua kuwa JK ni muumini safi wa strategic plan yaan mipango ya muda mrefu. Utakubaliana na mm kuwa baada ya kushinda mwaka 2005 JK alikuwa anajikita zaidi kutengeneza mipango ya muda mrefu ya kimaendeleo na ambayo ni sustainable. Utakubalina na mm kuwa mipango hiyo ndio inayowezesha kukamilika kwa utekelezaji wa ilani ya ccm ya mwaka 2010 kwa asilimia zaidi ya 85. Kutokana na kipindi hiki kuwa ni cha kutengeneza mipango kilishusha moral ya wananchi kwa CCM kidogo.
2. Sababu ya pili ya asilimia hizi kushuka ni ukweli usiopingika kwamba pamoja na kwamba muasisi wa sera ya UKWELI NA UWAZI ni MKAPA ila mtekelezaji wake mkuu alikuwa KIKWETE. Ndani ya miaka mitano ya JK mambo mengi maovu yaliwekwa wazi wananchi wakajua mfano UFISADI si kwamba huko nyuma lilikuwa halipo lilikuwepo toka enzi za Nyerere ila kulikuwa hakuna fursa za kujua mambo hayo, kuingia kwa JK madarakani na kuvipa vyombo vya habari uhuru zaidi ndio chamnzo cha haya mambo kujulikana. Kutokana na hali hiyo na kutokana na wananchi kuamini kuwa viongozi wao ni wema kimaadili wakati wote walipokuja kugundua kuwa baadhi yao ni wanyonyaji walikichukia chama na kutaka kulipiza kisasi kwa kumchagua slaa wakiamini kuwa ni padre na hawezi kuwanyonya. Ikumbukwe kuwa JK alilifanya hili kwa nia njema tu ya kutaka kuleta uwajibikaji (accountability ).
Nadhiriki kusema kuwa si kwa kuwa upinzani ni bora zaidi ndio ulioleta tofauti hii ya mwaka 2005 na 2010 bali ni RISK alizozibeba JK katika kuileta ccm mpya na tunayoitaka.
Kuelekea mwaka 2015 dalili zote za awali zimeshaonyesha kuwa CCM ndiye mshindiwa uchaguzi huo hata wakinisimamisha mimi hapa nitashinda. Hili limeonwa hata na wanachadema wenyewe na hata mtunga ilani yao ya mwaka 2010 dr KITILA ameliona. Katika andiko lake alilolipa jina la “CCM is stabilising, CHADEMA is shrinking and CUF is disappearing!” andiko la tarehe 11th February 2014 mwanazuoni huyu amejaribu kuonyesha jinsi chama chake kinavyokufa taratibu huku watawala wa ndani ya chama wakijaribu kuwaficha wanachama ukweli. Bila kuficha anachokiamini dr Kitila alikuwa akiwataka wanachama pamoja na vongozi wa CDM kutumia matokeo ya chaguzi ndogo wa kuanzia mwaka 2010 hadi 2014 kujipima na kujitathimini QUNTITAVELY kama chama kina gain au kina lose. Msomi huyu akitumia uchaguzi wa madiwani wa kata 27 wa mwezi wa pili 2014 amechambua matokeo yale quantitavely na kuonyesha ni kwa namna gani CDM inasinyaa kila kukicha huku CCM ikiimarika kwa kasi ya ajabu. Mfano kwa kutumia uchaguzi huo kati ya kata 27 CCM ilishinda kata 23 huku chadema ikiambulia kata 3 na NCCR kata 1. Ukijumlisha idadi ya wapiga kura wote kwa kata zote CCM ilipata idadi ya kura asilimia 85 CDM asilimia 11 na NCCR asilimia 1. Matokeo haya yapo karibu mno na uchaguzi mkuu ujao 2015.
Dr kitila hakuishia hapo kuwathibitishia watanzania kuwa chadema inasinyaa msinyao wa karatasi ya nailoni iliyokutana na moto wa gesi alitumia matokeo ya mwaka 2012 ya kata 29 zlizogombewa katika uchaguzi huo uliofanyika November 2012 CCM ilishinda kata 22 CDM kara 5 huku kata mbili zikienda vyama vingine. Msomi huyu alitumia data hizi na kuzilinganisha na hizi za 2014 ndipo alipogundua kuwa CCM inaimarika kila kukicha wakati CDM ikisinyaa.
Hapa tukitumia tena matokeo ya ubunge kwenye majimbo mawili ya KALENGA na CHALINZE utaona kuwa kusoma kunamzidi mpiga ramli kwani Kitila anazidi kudhihirisha alichokisema tarehe 11/2/2014.
Kuelekea mwaka 2015 CCM imezidi kuimarika zaidi pale ilipobadilisha safu yake ya uongozi. Safu hii ikiwa na mtendaji mkuu katibu Kinana, naibu wake bara Mwigulu na mwenezi wa chama Nape imekuwa ni mwiba mchungu sana kwa upinzani. Wameshtukia hili wanakuja kwa sura ya UKAWA. Tumeshawasoma mapema nina wasiwasi hata idadi ya wabunge wenu itapungua mwaka 2015.
Pia ujio wa Mgombea Bora Magufuli akiwa anasaidiwa na mgombea mwenza wa kwanza mwanamke katika historia ya siasa za Tanzania ni Tishio jingine Ukawa.
Tunashuhudia kuondoka kwa key players wa UKAWA Lipumba na slaa hawa wanatoa tafsiri ya taswira mpya ndani ya Ukawa kuondoka kwao ni PIGO japokuwa wanajifariji.
Mwaka huu Ukawa wanasimamisha mgombea ambaye hata ideology ya chama anachogombea haijui nani ampe nchi?
TUSUBIRI TIME
T.MUSHI

Hakuna maoni