RAIS KIKWETE AWACHIA KILIO WABUNGE WA CCM,NI KUHUSU AHADI ZAKE ZA 2010,SOMA HAPO KUJUA
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala |
AHADI zilizotolea na Rais Jakaya Kikwete
wakati wa kuwania urais mwaka 2010, zimeonekana kuwatesa wabunge wengi wa CCM
kutokana na nyingi kutokamilika na hivyo kuwaweka njia panda katika uchaguzi
mkuu wa mwaka huu. Anaandika
Dany Tibason … (endelea).
Hali hiyo ilijitokeza bungeni leo
wakati wa kipindi cha maswali na majibu, ambapo wabunge wengi waliihoji
serikali ni lini ahadi hizo zitakamilika.
Mbunge wa Magu, Dk.
Festus Limbu (CCM) katika swali la nyongeza alitaka kujua ni lini serikali
itatekeleza mradi wa maji katika mji wa Magu.
Naye Mbunge wa
Kahama, James Lembeli (CCM) akauliza ni lini serikali itatimiza ahadi
mbalimbali za ukamilishaji wa miradi ya maji katika jimbo hilo.
“Kuna ahadi nyingi
ambazo zilitolewa na Rais Kikwete lakini cha kushangaza miradi hiyo
haijatekelezwa sasa ni lini serikali itaweza kukamilisha ahadi hizo.
“Naitaka serikali
itoe kauli ni lini itaweza kutekeleza ahadi hizo ili wananchi waondokane na
adha ya maji ambayo inawafanya kushindwa kufanya shughuli nyingine za
kimaendeleo? Amehoji Lembeli.
Awali katika swali
la msingi la mbunge wa Magu, alitaka kujua ni lini serikali itatekeleza ahadi
ya kuwapatia maji ya uhakika wananchi wa mji wa Magu na ahadi hiyo imefikia
wapi.
Akijibu maswali
hayo, Naibu Waziri wa Maji, Amoss Makala, amesema ahadi zote zilizotolewa na
Rais zitatekelezwa.
Hata hivyo, amesema
tatizo kubwa ambalo linasababisha miradi kutokutekelezeka kwa wakati ni
kutokana na ufinyu wa bajeti.
Amesema serikali
imekuwa ikijitahidi kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inatekelezeka
japo changamoto kubwa ni ukosefu wa fedha ya kutosha.
Kwa hisani ya mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni