HABARI KUBWA LEO -MBATIA AIBOMOA BAJETI 2015/2016,ASEMA NI BAJETI LIPUA LIPUA SOMA HAPO KUJUA
Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, James Mbatia |
KAMBI Rasmi ya Upinzani Bungeni kupitia kwa Waziri Kivuli wa Fedha na
Uchumi, James Mbatia, imesoma bajeti mbadala wa ile iliyowasilishwa na
Serikali, huku ikiainisha masuala kadhaa ya kukuza uchumi na kupunguza
utegemezi…Anaandika Mwandishi Wetu … (endelea).
Kwa mujibu wa Mbatia aliye Mbunge wa
Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa NCCR-Mageuzi, katika kipindi cha miezi
minne ijayo kuanzia sasa, Serikali ya CCM ianze kujiandaa kisaikolojia
kuondoka madarakani na kupiisha kwa amani serikali adilifu itakayoongozwa na
UKAWA kuingia madarakani ili waweze kuwatumikia Watanzania.
Akiwasilisha maoni ya
upinzani leo kwa Bajeti ya 2015/16, Mbatia amesema “tunapendekeza kukusanya Sh.
bilioni 19,695.2 ambapo mapato ya kodi na yasiyo ya kodi Sh. bilioni 18,847.1
(sawa na asilimia 20) ya Pato la Taifa.”
Aidha, mapato ya
halmashauri ni asilimia 0.9 ya pato la Taifa sawa na Sh. bilioni 848.1.
Amesema hiyo ni bajeti isiyo
na mikopo ya kibiashara, hivyo inalenga kulipunguzia taifa mzigo wa madeni,
tofauti na ile ya serikali yenye mikopo ya masharti ya kibiashara ya 10%
na hivyo kuwaongezea wananchi mzigo wa madeni.
“Bajeti inayoendelea
kusisitiza umuhimu wa kuwalipa pensheni wazee wote nchini wenye umri wa miaka
60 na kuendelea wakati ile ya serikali iko kimya kabisa kuhusu malipo ya
pensheni kwa wazee wote nchini, kwani bado inaendelea kufanya upembuzi yakinifu
usioisha,”amesema.
Mbatia ameongeza kuwa bajeti
yao inaendelea kusisitiza kushusha kiwango cha tozo ya kodi ya mapato ya ajira
kwa wafanyakazi (PAYE) hadi kufikia asilimia 9 badala ya 11 ya serikali
inayokandamiza wafanyakazi.
Kuhusu vyanzo vipya vya
mapato ya ndani, upinzani umeainisha na hivyo kuonesha kuwa ni nchi
inayojitegemea kwa asilimia 89.5 wakati ya serikali ni tegemezi kwa
asilimia 10.32 kutokana na kukopa kwa kiwango kikubwa na hivyo kuongeza deni la
taifa.
Mapato ya ndani ya kodi na
yasiyo ya kodi, Mbatia anasema yatakuwa asilimia 20 ya pato la Taifa kinyume na
serikali yenye mapato ya ndani ya kodi na yasiyo ya kodi asilimia 14.3 ya pato
la Taifa.
“Bajeti yetu inalenga
kupunguza misamaha ya Kodi hadi kufikia asilimia 1 ya Pato la Taifa ili kuongeza
mapato ya ndani wakati serikali imetaja tu azma ya kupunguza misamaha ya kodi
bila kufafanua kwa undani.
“Tunalenga kutekeleza
kikamilifu miradi ya maendeleo kwa kutenga asilimia 27.34 ya bajeti yote
kugharamia miradi ya maendeleo. Bila kukopa katika mabenki ya ndani wakati
asilimia 26.31 ya bajeti ya serikali ni matumizi ya maendeleo. Hii ni pamoja na
kukopa kibiashara katika
mabenki ya ndani,” amesema.
Mbatia ameongeza kuwa, bajeti yao inalenga kukusanya mapato kutoka kwenye
vyanzo ambavyo havimuumizi mwananchi wa kawaida tofauti na serikali inayolenga
kukusanya mapato kutoka katika bidhaa zinazotumiwa kila siku na wananchi hivyo
kuongeza ugumu wa maisha.
Anasema “matumizi ya
kawaida yatakuwa ni asilimia 72.66 ya bajeti yote baada ya kutenga fedha za wazee
na kuongeza mishahara kwa 10% huku ile ya serikali matumizi ya kawaida ni
73.69.”
Kwa mujibu wa Mbatia, bajti
yao ni ya kumsaidia mwananchi wa kawaida kutoka katika wimbi la umaskini,
tofauti na ile ya serikali ya CCM aliyosema haimtambui mwananchi maskini na
kuongeza matumizi makubwa kwa watawala.
Kuhusu ongezeko la bei ya
mafuta, Mbatia amesema, “ni suala mtambuka litakasababisha mfumuko mkubwa wa
bei na hatimaye kuongeza uchungu na ugumu wa maisha ya Mtanzania kwa sababu bei
za usafiri na bidhaa za mazao zinazosafirishwa kutoka eneo moja kwenda eneo
jingine pia zitapanda
Habari hii imeandaliwa kwa hisani ya Mwanahalisi oline
Hakuna maoni
Chapisha Maoni