Zinazobamba

ZAIDI YA WATU 30 WAFARIKI KATIKA AJARI YA KONTENA NA BASI HUKO ILINGA

Watu zaidi ya 30 wanasadikiwa kupoteza na maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya sana katika ajali mbaya iliyotokea mapema leo asubuhi,maeneo ya Changarawe,Mafinga Mkoani Iringa,iliyohusisha Lori la Mizigo na Basi la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitokea Mkoani Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam.


Hali ya Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hiyo bado ni tete na hasa kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi hilo kukosekana eneo lote la Mafinga,Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti.


Ajali hiyo imetokea baada ya Lori hilo la Mizigo lililokuwa likitokea Jijini Dar kuelekea Mbeya kuligonga na kuliangukia basi hilo wakati lililokuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara wakati wakiwa kwenye mwendo walipokuwa wakipishana.

Tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu tukio hili ambalo ni la kusikitisha sana na ni msiba mkubwa kwa taifa,na tutaendelea kujuzana kupitia hapa hapa.

Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.

Hakuna maoni