WAHISANI SASA WAKUBALI KUACHIA FEDHA,- NI BAADA YA KURIDHISHWA NA SAKATA LA ESCROW
Wadau wakimsikiliza waziri wa fedha pindi alipokuwa akifafanua jambo kuhusu wahisani kuachia fedha kwa serikali ya Tanzania. |
Kufuatia hatua ambazo serikali
zimeshughulikia sakata la Escow, sasa wadau wa maendeleo na benki ya Dunia
wamewkubali kwa kauli moja kuachea fedha kwa serikali ya Tanzania katika bajeti
ijayo ili serikali iweze kupanga mipango yake vizuri,
Akizungumza na waandishi wa habari
mapema hii leo, Waziri wa Fedha , Mh. Saada Mkuya amekili kuwa sasa wahisani
wamekubali kuachia fedha ,ili serikali ipange mipango yake ya kimaendeleo
pasipo kikwazo kutoka kwa wahisani,
Mkuya amesema hatua ya wahisani kukubali
kutoa fedha hiyo inatokana na wahisani hao kuridhishwa na hatua ambazo serikali
imezichukua katika kushughulikia sakata la Escrow ambalo limekuwa sababu ya wao
kusitisha misaada kwa serikali,
Mkuya ameendelea kusema kuwa Kwa
jinsi ambazo wamekubaliana Wahisani hao wataanza kuachia jumla ya Dola 44
Milion kwanza na baadaye wataziachia
fedha nyingine ambazo kimsingi walikubaliana kuzitoa katika serikali ya
Tanzania,
Nao banki ya Dunia imeahidi kutoa
fedha Takribani Dola Milion 227 kwa serikali ya Ttanazania hapo baadae ili
kusapoti bajeti ijayo
Ilikuwa ni Alhamisi, Novemba 6, 2014, Waziri mkuu
hakusita kuonyesha masikitiko yake na ya nchi yetu kwa ujumla kwa kitendo cha
wahisani kuzuia misaada ya Jumuiya ya Ulaya zikiwamo pia Norway, Canada, Japan,
Benki ya Dunia na hata Benki ya Maendeleo ya Afrika.
Wahisani hao walisitisha kutoa fedha
kwenye Bajeti Kuu, kiasi cha dola za Marekani 558 sawa na shilingi bilioni 937
ambazo sasa baada ya kuridhishwa wameamua kuachia fedha hizo kwa serikali yetu
Kulikuwa na maneno mengi sana
yalisemwa juu ya wahisani kusitisha fedha hizo,wengine walifika mbali na kusema
kwamba wahisani hao wanaamua bila
kufanya mazungumzo ya kina na wanaowahisani. Laiti wahisani wangekaa chini na
Serikali kuzungumzia azma yao ya kusitisha misaada yao kwa bajeti kuu, naamini,
kuwa wangepata ufahamu mkubwa juu ya mchakato wa sakata hilo ulivyo, na kwamba
wangevuta subira kusubiri matokeo ya mchakato huo. Sasa mambo yamekaa sawa,
fedha zitatoka tu kama walivyokubaliana.
Wafadhili wa mataifa ya nje kwa
Tanzania walisimamisha misaada yao kwa serikali ya Tanzania wenye thamani ya
karibu Dola za kimarekani Milioni 558 sawa na Pauni za kiingereza Milioni 311
ambazo zingetumika katika kusaidia bajaeti ya Taifa.
Hatua hiyo ilikuja kufuatia madai ya
ufujaji wa pesa unao walenga baadhi ya maofisa wa juu wa serikali ya Tanzania
wanaotuhumiwa kuchota kiasi cha pesa kutoka katika Benki kuu kwa kivuli cha
mikataba ya Nishati.
Mbunge wa Kigoma Mh. Zitto Kabwe ambaye
pia ni mwenyekiti wa kamati ya PAC ndiye alipigilia msumari wa sakata hilo
baada ya kusema kuwa maofisa kadhaa wa ngazi za juu serikalini walishirikiana
na wafanya biashara wabadhirifu kuhamisha kiasi cha Dola Milioni 122 kutoka
katika Benki Kuu ya Tanzania kwenda katika akaunti ya Benki binafsi.
Wahisani wanaosaidia bajeti ya
Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja
wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki
ya Dunia.
Antila aliongeza kuwa "Serikali
ya Uingereza haina uvumilivu kwa rushwa na udanganyifu, na kwa kushirikiana na
wahisani wengine, haitofadhili bajeti nyingine yeyote kwa Serikali ya Tanzania
mpaka tutakapoona madai haya yanashughulikiwa na serikali ipasavyo".
Benki ya Dunia na wahisani wengine
kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani
ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 230.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni