HABARI KUBWA LEO- MPANGO WA KUMUUA DK SLAA,MLINZI WAKE ALIPUKA.AMWAGA UGALI,AFICHUA MADUDU,SOMA HAPA
Pichani ni Aliyekuwa Mlinzi wa Dokta Slaa, Bwana Khalid Kagenzi akuzingumza na Waandishi wa Habari mda huu |
Pichani Mlinzi wa Kagenzi akionyesha mateso aliyofanyiwa na Makada wa Chadema |
SIKU chache kupita baada ya Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Mabere Marandu
kufichua njama za Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana
Khalid Kangezi kupanga-
Mipango ya kumuua katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo wa
Chama Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni,naye
Mlinzi huyo bwana Kagenzi ameibuka kufichua siri nzito ndani ya Chama hicho
kikuu cha upinzani nchini.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo hapo.
Akifichua
siri hiyo Mda huu Jijini Dar es Salaam Mbele ya Waandishi wa Habari amesema
anasikitika sana na madai ya uongo yanayoenezwa na viongozi wa Chadema huku
wakifacha ukweli wa Mambo kwani ukweli way eye kuzushiwa uongo huo unatokana na
kuwa na mahusiano na Mke wa Dokta Slaa .
“Leo nashangaa sana hawa Viongozi
hawa wa Chadema wanaosema mimi ni nimehusika katika mipango ya kumuua Slaa,wanaficha
ukweli kwani sababu yote hii ya kuzushiwa uongo inatokana na mimi kuwa na
mahusiano mabaya na Mke wa Slaa,nilipoenda kumwabia Slaa”
“na akasema niende kumalizana na mke wake lakini ukweli na mke wake mambo
hayakwenda vizuli ndipo hapo Slaa akapeleka kwenye uongozi wa juu”amesema
kagenzi.
Akionyesha Vidonda |
“
Mlinzi Kagenzi ameongeza Mala baada ya Dokta Slaa kupeleka ugomvi huo
kwenye ngazi za juu,ndipo yeye siko moja anakuja ofisini akakamatwa na
kupelekwa kwenye chumba cha utesaji ambacho anadai kinamilikiwa na chama hicho.
Bwana Kagenzi ameendeleo kusema kuwa
hata madai wanayodai kwamba anahusiano wa karibu na usalama wa Taifa pamoja na
Vigogo wa CCM anadai ni ya uongo mkubwa kwani
hana mahusiano na watu hao.
“Jamani hivi inaingia akilini kweli
mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni
uwongo wa hali ya juu.na wanataka kunichafua kwa jamii,tena niseme ukweli chama
hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.”
“Ni kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa dokta
slaa kwa mda wa miaka mingi sana ,tena mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi
chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua huo ni unafiki”amesema Kagenzi
Katika Jambo la kushangaza Mlinzi huyo amefuchua mipango
ya kitesaji na kigaidi inayofanya na Chadema huku akisema wameandaa ofisi ya utesaji.
“Jamini hiki chama ambacho kinandoto ya
kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia
maana wameniteka na kunifungia kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao
wamechoma visu.na kuweka kwenye Mashine ya
umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza mimi nitaje wanaonituma,jamani
nawaambia mimi anitumi mtu”ameedelea kusema Kagenzi.
Aidha,Kagenzi amekitupia lawama chama
hicho huku akisema kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume
.
Alibanisha kuwa hata alivyokuwa mlinzi
wa Dokta Slaa kwa miaka mitano zaidi alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu
kwa mwezi lakini anasema kuwa hakuandaa
mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini leo wanamsingizia kiasi
hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka kufanya vitendo vya kukisaliti
chama angefanya huko nyuma.
Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu
yake na watu wa Usalama wa Taifa.
Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo
zinazosemwa kwani hata simu yake haina salio ya pesa na haijawai kupokea pesa
hizo.
Hatua anachukua.
Kagenzi
amesema hatua iliyopaki sasa hivi ni kwamba tayari ameshahojiwa na jeshi la
Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubili kesi mahakamani,ili kukishtaki chama
hicho kwa Vitendo walivomfanyia navyodai
ni vya kiuwaji.
Maoni 2
Vingozi wengi wanapotaka kuficha makucha yao wanatumia vivuli vya wanyonge
www.pambazukaclassic.blogspot.com
Chapisha Maoni