Zinazobamba

HABARI KUBWA LEO- MPANGO WA KUMUUA DK SLAA,MLINZI WAKE ALIPUKA.AMWAGA UGALI,AFICHUA MADUDU,SOMA HAPA

Pichani ni Aliyekuwa Mlinzi wa Dokta Slaa,
Bwana Khalid Kagenzi
akuzingumza na Waandishi wa Habari mda huu
Pichani Mlinzi wa Kagenzi akionyesha mateso aliyofanyiwa na 
Makada wa Chadema
      

 SIKU chache kupita baada ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Mabere Marandu kufichua njama za Mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilbroad Slaa, bwana Khalid Kangezi kupanga-
  Mipango ya kumuua  katibu huyo huku akishirikiana na Vigogo wa Chama Mapinduzi CCM pamoja na Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Kinondoni,naye Mlinzi huyo bwana Kagenzi ameibuka kufichua siri nzito ndani ya Chama hicho kikuu cha upinzani nchini.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo hapo.
      Akifichua siri hiyo Mda huu Jijini Dar es Salaam Mbele ya Waandishi wa Habari amesema anasikitika sana na madai ya uongo yanayoenezwa na viongozi wa Chadema huku wakifacha ukweli wa Mambo kwani ukweli way eye kuzushiwa uongo huo unatokana na kuwa na mahusiano na Mke wa Dokta Slaa .
           “Leo nashangaa sana hawa Viongozi hawa wa Chadema wanaosema mimi ni nimehusika katika mipango ya kumuua Slaa,wanaficha ukweli kwani sababu yote hii ya kuzushiwa uongo inatokana na mimi kuwa na mahusiano mabaya na Mke wa Slaa,nilipoenda kumwabia Slaa”
 “na akasema niende kumalizana na  mke wake lakini ukweli na mke wake mambo hayakwenda vizuli ndipo hapo Slaa akapeleka kwenye uongozi wa juu”amesema kagenzi.
Akionyesha Vidonda
      Mlinzi Kagenzi ameongeza  Mala baada ya Dokta Slaa kupeleka ugomvi huo kwenye ngazi za juu,ndipo yeye siko moja anakuja ofisini akakamatwa na kupelekwa kwenye chumba cha utesaji ambacho anadai kinamilikiwa na chama hicho.
        Bwana Kagenzi ameendeleo kusema kuwa hata madai wanayodai kwamba anahusiano wa karibu na usalama wa Taifa pamoja na Vigogo wa CCM anadai  ni ya uongo mkubwa kwani hana mahusiano na watu hao.
            “Jamani hivi inaingia akilini kweli mimi leo na maisha yangu haya niwe na uhusiano na watu wa usalama na CCM,huu ni uwongo wa hali ya juu.na wanataka kunichafua kwa jamii,tena niseme ukweli chama hiki kinataka kuficha ukweli juu ya mambo waliyonitendea.”
       “Ni kwamba mimi nimekuwa mlinzi wa dokta slaa kwa mda wa miaka mingi sana ,tena mimi nilikuwa nampikia na kumtengea hadi chai ya kunywa eti leo niambiwe naandaa mipango ya kumuua  huo ni unafiki”amesema Kagenzi
        Katika Jambo  la kushangaza Mlinzi huyo amefuchua mipango ya kitesaji na kigaidi inayofanya na Chadema huku akisema wameandaa ofisi  ya utesaji.
     “Jamini hiki chama ambacho kinandoto ya kuchukua nchi leo kinaandaa mipango ya mauaji na utesaji kama walivyonifanyia maana wameniteka na kunifungia kwenye chumba cha utesaji wanachomiliki wao wamechoma visu.na kuweka kwenye Mashine  ya umeme bila kosa lolote,eti wakinishinikiza mimi nitaje wanaonituma,jamani nawaambia mimi anitumi mtu”ameedelea kusema Kagenzi.
     Aidha,Kagenzi amekitupia lawama chama hicho huku akisema kwenye mateso waliyomtesa yamemfanya apoteze hata nguvu za kiume .
        Alibanisha kuwa hata alivyokuwa mlinzi wa Dokta Slaa kwa miaka mitano zaidi alikuwa analipwa malipo madogo ya Laki tatu kwa  mwezi lakini anasema kuwa hakuandaa mipango ya yoyote ya kumuua,lakini anashangaa kwanini leo wanamsingizia kiasi hicho kwani amedai kuwa kama angekuwa anataka kufanya vitendo vya kukisaliti chama angefanya huko nyuma.
    Kuhusu kuingiziwa Milioni saba kwenye simu yake na watu wa Usalama wa Taifa.
  Kagenzi amesema hizo ni taarifa za uongo zinazosemwa kwani hata simu yake haina salio ya pesa na haijawai kupokea pesa hizo. 
   Hatua anachukua.

Kagenzi amesema hatua iliyopaki sasa hivi ni kwamba tayari ameshahojiwa na jeshi la Polisi na kilichobaki sahivi ni kusubili kesi mahakamani,ili kukishtaki chama hicho kwa Vitendo  walivomfanyia navyodai ni vya kiuwaji.






Maoni 2

Unknown alisema ...
Maoni haya yameondolewa na mwandishi.
Unknown alisema ...

Vingozi wengi wanapotaka kuficha makucha yao wanatumia vivuli vya wanyonge
www.pambazukaclassic.blogspot.com