Zinazobamba

WENGINE WAKITIMUANA,KINANA WA CCM,AKIJENGA CHAMA CHAKE,MSHUHUDIA HAPA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (katikati), akishiriki kuchimba shimo la choo cha Shule Mpya ya Msingi ya Kikwete, eneo la Chamwino Ikulu, Jimbo la Chilonwa wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua miradi inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, katika Wilaya ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa chombo chenye dawa aliposhiriki kupulizia dawa za kuua wadudu katika mradi wa shamba la zabibueneo la Chinangali 11, Wilaya ya Chamwino jana.
 Komredi Kinana akishiriki kupulizia dawa ya kuua wadudu katika mradi wa shamba la zabibu wa Chinangali 11, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma jana.
 Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kupitia Vijana, Deo Ndejembi wakishiriki kupulizia dawa za kuu wadudu katika shamba la zabibu la Chinangali 11, wilayani Chamwino, mkoani Dodoma jana.
Zao la zabibu katika shamba hilo. Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi akishiriki kuchimba shimo la choo cha Shule mpya ya Msingi ya Kikwete, Chamwino Ikulu, jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni Chiku Galawa (kushoto), Katibu wa CCM Wilaya Chamwino, Janeth Masheli (katikati) na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi wakiwa na furaha baada ya kuona Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuchimba kisima cha Shule ya Msingi ya Kikwete, Chamwino Ikulu jana.
 Komredi Kinana akipanda mti  mbele ya Ofisi ya Wilaya ya Chamwino inayojengwa.
 Komredi Kinana akiingia ukumbini kuendesha mkutano wa Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Chamwino.
 Mmoja wa walimu akitoa ushauri kwa Komredi Kinana, kuanzisha utaratibu wa kuwapa somo vijana kujua historia ya CCM, ikiwa ni sehemu ya kuwaanda kuja kushika madaraka ya chama na nchi.
Mjumbe wa Halmashauru Kuu ya Taifa ya CCM Deo Ndejembi akishiriki kutoa mchanga wakati wa kuchimba shimo la choo cha choo cha Shule ya  Msingi ya Kikwete, wilayani Chamwino.Nyota njema Kikundi cha ngoma za asli ya kabila la Wagogo linaloshirikisha watoto wanaopiga kwa ustadi ngoma kikitumbuiza baada ya Kinana kuwasili  kushiriki ujenzi wa Shule ya Msingi ya Msanga B, wilayani Chamwino.Katikati ni mtoto Jamima Juma mwenye umri wa miaka mitatu.
 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa vymba vya madarasa vya Shule ya Msingi ya Msanga B, wilayani Chamwino jana.
 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Mahampha katika Kata ya Chilonwa, wilayani Chamwino jana.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiungana na vikundi vya ngoma kupiga ngoma alipowasili kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Majereko, wilayani Chamwino jana.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Luteni Chiku Galawa na Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Farida Mgomi  wakishiriki kupiga ngoma wakati vikundi vya ngoma za utamaduni zikimlaki Katibu Mkuu wa CCM, Kinana kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Majereko, Chamwino.
Kikundi cha ngoma za asili ya kabila la Wagogo cha Nyota kikitumbuiza katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari ya Majereko.
 Wasanii wa Kikundi cha Nyota kifanya maajabu kilipokuwa kikitumbuiza katika mkutano huo.
 Kikundi cha ngoma za utamaduni wa asili wa Kabila la Wagogo cha Simba kikitumbuiza wakati wa mkutano huo.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katikahuo wa  mkutano wa hadhara.
 Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana akihutubia katika mkutano huo, ambapo alisema CCM ni chama pekee nchini kinachowajali wanawake kwa kuwapatia nafasi nyingi za uongozi. Leo ni masdhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo kitaifa imeadhimishwa mkoani Mororo na mgeni rasmi alikuwa Rais Jakaya Kikwete.ikukuu ya kudhimisha.
Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana akimpatia sh. 500,000 Katibu wa CCM,Wilaya ya Chamwino, Janeth Masheli za kuwagawia zawadi wasanii wa vikundi kumi vya ngoma za utamaduni vilivyotumbuiza katika mkutano huo.

Hakuna maoni