Zinazobamba

NAIBU WAZIRI MBENE AWAHASA WATANZANIA,AWATAKA WAACHE KUBWETEKA SOMA HAPA KUJUA


NAIBU  Waziri wa Viwanda na Biashara, , Mheshimiwa Janeth Mbene (pichani) amewataka watanzania kuacha kulalamika kwa kukosa Ajira badala yake amewahasa kujihusisha katika Fursa nyingi zilizopo nchini ikiwemo kwenye Bidhaa ndogondogo.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo.
Naibu Waziri Mbene ameitoa kauli hiyo leo Jijini Dar Es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa masuala ya uchumi na uwekezaji ili kuzungumzia Fursa ziliopo hapa nchini na nini wa kifanye kumwokoa mtanzania ambapo amesema ni wakati wa Vijana kuacha kulalamika na kuanza kujiingiza katika mipango ya kukuza biashara.
    “Nashangaa sana leo watanzania wanalalamika kwa kukosa kazi,lakini inashangaza sana kwamba wenzetu wa nchi jirani ikiwemo kenya wameziona fursa hapa nchini,kwa mfano nilipokuwa Dubai nilimkuta mwanamama Mkenya akiuza bidhaa za Tanzania huku akizitambulisha ni za Kenya,na anapata soko kubwa sana sasa nashangaa kwanini fursa hii isiwe kwa watanzania”amesema Waziri Mbene.
           Naibu Waziri Mbene ameongeza kuwa kwa sasa Wizara yake katika kuendeleza mpango wa Matokeo Makubwa sasa yaani (Big result now)kwa sasa wameviweka vipaumbele mbali kwa watanzania kujikwamua katika Dimbwi la Umasikini.
      Aidha,Naibu waziri Mbene amesema katika kuonyesha wanania ya kuwavutia wawekazaji hususani wanaotaka kuja nchini na kuwekeza kwenye bidhaa ya matunda kwa sasa wako mbioni kuanzisha soko pekee litakarojihusisha na uuzaji wa matunda peke yake ili kufanya wawekezaji wajivunie kuja hapa nchini.

        Vilevile,Naibu huyo akawataka watanzania kwenda na kasi ya  Maendeleo ya nchi kwa kuzifuata fursa zilizopo ikiwemo kwenye suala nzima la uekezaji kwa bidhaa ndogo ndogo.

Hakuna maoni