UKWELI KUHUSU KUFUKUZWA MCHEZAJI MRANDWA NA NIYONZIMA KLABUNI YANGA,SOMA HAPA KUJUA
KLABU ya
Soka ya Yanga imekanusha taarifa
zilizozagaa mitaani na kwenye Mitandao ya Kijamii kwamba klabu hiyo imewafukuza wachezaji wake wawili ambao ni
Danny Mrwanda na kiungo wake Haruna
Niyonzima kutokana na timu hiyo kupoteza mechi yake na Simba iliyochezwa mwishoni mwa
wiki iliyopita Anaandika KAROLI VINSENT, Endelea nayo.
Akikanusha taarifa hizo leo
Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari ,Mkuu wa kitengo
cha Habari wa Klabu wa Yanga Jerry Murro ambapo amesema klabu hiyo haijamsimamisha
mchezaji wake wala kumuita na kumuhojai kutoka na mechi ya simba.
“ Sisi
viongozi baada ya mechi ya simba atukuzungumza na wachezaji wetu yeyote kabisa,tena
ni mapema sana kuzungumzia hali hiyo kwani hilo ni suala ni la benchi ya ufundi
na hakuna kitu kama hicho cha kufukuzwa
mchezaji“amesema Murro
Murro ameongeza kuwa kwa hao
wachezaji ambao wanadaiwa kwamba wamefukuzwa akimtaja Danny Mrwanda amesema
mchezaji huyo anaumwa kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Maralia na Daktari
wa timu hiyo amethibitisha ugonjwa wake
na pia mchezaji huyo amepata kadi nyekundu kwenye mechi iliyopita ya Kimataifa.
Aidha,Afisa habari huyo akawataka
wanachama na mashabiki wa Yanga kupuuza taarifa zinazoenezwa zenye nia mbovu ya kupotosha umma.
Katika hatua nyingine Klabu hiyo
yenye maskani yake Jangwani jijini Dar es Salaam imetangaza rasmi kiingilio
kati ya mechi yake ya kombe la shirikisho barani afrika na timu ya Fc Plantim
inayotarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki hii ambapo kwa mujibu wa jerry murro
Amesema Tiketi
za mchezo huo zitauzwa siku ya jumamosi na tiketi zitakuwa katika mafungu
mawili ambapo ni tiketi za elfu tano na elfu thelasini,
Hakuna maoni
Chapisha Maoni