MZIMU WA KOMBA WAMTESA LOWASSA,BADO ANAWEWESEKA NA KIFO CHAKE SOMA HAPA KUJUA
WIKI
moja tangu Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba (CCM) afariki dunia,
Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ameendelea kumlilia akimtaja kama
mmoja wa makamanda wa kuongoza harakati za kumshawishi awanie urais. Anaandika
Mwandishi wetu…(endelea).
Kabla
ya kukumbwa na mauti, marehemu Komba alijipambanua kama mshirika mkubwa wa
Lowassa, aliyeapa kumpigania ndani ya CCM kuhakikisha anagombea urais mwaka
huu, akidai ndiye anayestahili kumrithi Rais Kikwete.
Katika kujipambanua huko kumpigania Lowassa agombee urais, maremu
Komba alikaririwa akitamba kuwa tayari alikuwa ametunga nyimbo tatu kwa ajili
ya kumnadi kada huyo ambaye hata hivyo hajatangaza rasmi kama ataingia kwenye
kinyang’anyiro hicho.
Kutokana na ukaribu wa wawili hao, Lowassa kupitia kwa msaidizi
wake, leo amesambaza taarifa ya tanzia yake kwa Komba akismea; “Ulipaza sauti
bila woga kuelezea imani yako kwangu. Kapteni naumia sana umeondoka bila ya
kukupa jibu la kukubaliana na ushawishi wako au la.
Tanzia ya Lowassa kwa Komba
>>>> Hivi ni kweli
sitosikia tena sauti yako Captain Komba!, mbona umeondoka bila ya kuniaga ndugu
yangu! Moyo wangu unabubujika machozi ya damu.
>>>>
>>>> Maneno yako kwa mmoja wa wasaidizi wangu siku tatu kabla ya umauti kukupata kwamba “mwambie Edward akija aje kuniona mimi sijisikii vizuri” yanazunguka akilini mwangu.
>>>>
>>>> Captain Komba, Mimi na wewe tumepigana vita nyingi kwa maslahi ya chama na nchi yetu…na tulishinda vita hivyo. Lakini bado tulikuwa tunaendelea na mapambano ya kumnasua mtanzania katika umasikini.
>>>>
>>>> Komba ulikuwa muumini usiyeyumba wa “Safari ya Matumaini”. Ulikuwa mmoja wa makamanda wa kuongoza harakati za kunishawishi niwanie urais kupitia chama chetu. Ulipaza sauti bila woga kuelezea imani yako kwangu. Captain naumia sana umeondoka bila ya kukupa jibu la kukubaliana na ushawishi wako au la.
>>>>
>>>> Kwa hakika chama kimepata pigo. Ni nani asiyejua mchango wako katika ushindi wa chama chetu katika ngazi zote. Nyimbo zako ndiyo adhana au kengele ya kuwakusanya waumini (wana ccm na wananchi) katika mikutano ya chama. Komba ulikuwa nembo ya chama chetu.
>>>
>>> Komba umeondoka lakini umeacha alama katika ulimwengu wa siasa hususan katika chama chetu. Daima nitakukumbuka ndugu yangu, naamini kabisa yale mapambano utayaendeleza huko ulikoenda ambako sote tutakuja.

>>> Nakuahidi ndugu
yangu kama tulivyokuwa pamoja katika matatizo na furaha zetu, mimi na chama
chetu tutaendeleza pale ulipoachia kutatua matatizo ya familia. Namuomba mungu
anipe nguvu na moyo wa kuyafanya hayo. Pumzika kwa amani rafiki yangu ipo siku
isiyo na jina tutaonana
Hakuna maoni
Chapisha Maoni