SERIKALI YA KIKWETE YASHIKWA PABAYA NA CHAMA CHA ADC CHAIBUKA NA WASEMA YA KWAO SOMA HAPA
Pichani ni Mwenyekiti wa Cha cha (ADC) Said Miraaj Abdulla Akizungumza na waandishi wa Habari mda huu Jijini Dar es Salaam |
CHAMA cha
kisiasa cha Alliance for Democratic Change(ADC)kimeitaka serikali ya Rais
Jakaya Kikwete kuwageukia watanzania waliokata tama na maisha kwa mfumo wanaodai
ni wakinyonyaji.
Aidha,Chama hicho pia kimesikitika kusuasua kwa serikali katika kutatua
matatizo yanayowakumba Watanzania ikiwemo
majanga mbalimbali ambayo yametokea hivi karibuni ikiwemo mauaji ya watu wenye
ulemavu wa ngozi wa Albino.Anaandika KAROLI VINSENT Endelea nayo
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar
es Salaam na Mwenyekiti wa chama cha ADC Taifa,Said Miraaj Abdulla wakati wa
mkutano na waandishi wa habari ili kuzungumzia hali ya masha kwa Watanznaia ambapo amesema hivi sasa nchini kuna matukio mengi ya vifo
vinavyoweza kuzuilika ambavyo anadai katika hali ya kawaida hakuna anaelalamika
kuomba vifo hivyo vikomeshwe.
“Kiukweli kunapotokea matatizo makubwa ikiwemo hili la
mvua ya mkoani kahama tumeshuhudia
viongozi mbalimbali wengine hudiriki hata kutoa rambirambi za mamilioni
kwa wafiwa ili waonekane kwenye luninga,hali ya kuwa marehemu hawajawai
kumuona,na huku mtoaji huyo huyo mrehemu hawajawai kumuona”amesema Abdulla.
Waandishi wa Habari wakiwa kazini |
Abdulla ameongezeka kuwa wananchi
wamekuwa wakikumbana na matatizo mengi lukuki ikiwemo tatizo la
umasikini,ajira,na tatizo la ombwe la uongozi huku serikali bado ikiwa
hajawaweka njia ya kutatizo.
Alaibainisha kuwa kwa kusema hadi lini wanyonge wataendelea kufa huku
akidai wakubwa wakifaidi matunda ya kutibiwa nje wao na familia zao tena kwa
gharama za kodi inayolipwa na masikini wanao kufa kwa maradhi mbalimbali.
Katika hatua nyingine chama chicho cha upinzani nchini kimesikitika kwa
kile wanachesema ni dharau kwa serikali iliyopo madarakani kwa kitendo chake
cha kushindwa kuwachukulia hatua watendaji mbalimbali waliopelekea hadi kutokea
kwa ajali mbaya gari iliyotokea juzi mkoani Iringa na kupolekea vifo vya watu
zaidi ya 48.
‘Hii ni
serikali gani isiyokuwa na uchungu kwa wananchi ni serikali gani isiyoshtuka na
vifo vya watu zaidi ya 48,huko iringa leo tumemsikia mkuu wa mkoa huo akisema
basi lilobeba abiria lemezidisha watu,hivi jamani hebu tujiulizeni ilo basi
limepita maeneo mbalimbali huku polisi wabarabarani wakiliangalia tu,kama hii
ingekuwa serikali makini –“
“Ingechunguza pindi basi hilo linapita maeneo yote mpaka linapata
ajali na lingechunguza nani alikuwepo barabarani na nani alikuwa kwenye vituo vya uchunguzi na
wangechukuliwa hatua maana hapa kuna mambo ya Rushwa “amesema Abdulla.
Vilevile,Abdulla amelitupia Lawama
jeshi la Polisi nchini kwa kitendo chake cha kuwafedhehesha wananchi ambao
wanatuhumiwa na matukio mbalimbali ya uharifu kuwaonyesha kwenye luninga kuwa
ni watuhumiwa bila ya kuwa na ushahidi huku watuhumiwa hao wakipelekwa
mahakamani wanashinda kesi na jeshi la polisi halirudi kwasafisha kama
limewakuta hawana makosa.
Bwana Abdalla ametoa wito kwa watanzania
kutovumilia hujuma zinazofanywa na
serikali badala yake amesema ni wakati wa kuacha kulalamika ni mda wakufanya
maamuzi magumu kuindoa serikali iliyoko madarakani.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni