EXCLUSIVE--TAPELI WA IKULU YA KIKWETE AKAMATWA,ABAINIKA KUWATAPELI VIGOGO.SOMA HAPA KUJUA
JESHI la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata tapeli maaufu hapa jijini anayeitwa Haroub Mtopa miaka 44 mkazi wa mbagala rangi tatu ambaye amekuwa akiwatapeli watu
mbalimbali kwa kutumia jina la Katibu wa
Rais Jakaya Kikwete, Prosper
Mbena kuwatapeli wananchi mbalimbali.Anaandika KAROLI
VINSENT,Endelea nayo.
Akithibitisha kumkamata
tapeli huyo leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa mkutano na waandishi wa
Habari,Kamishna wa kanda maalum ya polisi Mkoa wa Dar es Salaam,kamishna
Suleiman Kova amesema mtu huyo alikamatwa na maofisa wa usalama walioko Ikulu
ambapo walimnasa kutokana na yeye kuwa na tabia ya kwenda ikulu hapo mara mara
kwa bila ya kutokuwa na kazi yeyote.
Kamishna Kova ameongeza kuwa tapeli
huyo amekuwa na tabia kwenda na wananchi mpaka nje ya mlango wa kuingia wa ikulu na
kuwaacha nje huku akijifanya anaingia ndani ikulu ili kuwaaminisha wananchi hao
kwamba anafanya kazi ikulu.
Pichani ni Kamishna Kova |
Aidha,kamishna Kova
amesema mtu huyo amekuwa akizitapeli ofisi mbali mbali za Kiserikali kwa
kutumia njia hiyo ya kutumia jina la Mbene pamoja na wananchi.
Vilevile Kamishna Kova
amesema siku ya kumkamata walimwekea mtego ndipo ikawa rahisi wao
kumkamata.ambapo kamishna kova akawataka wananchi kuwa makini na watu wa aina
hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni