HABARI KUBWA LEO-MAASKOFU WAISUSA CCM,NI KUHUSU MAHAKAMA KADHI,WASEMA LIWALO NA LIWE,SOMA HAPA KUJUA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete |
JUKWAA la Wakristo nchini limetaka waamini wake, kutopigia kura
Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani,
unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu. Anaandika Saed Kubenea…(endelea).
Uamuzi wa kutaka waamini wa madhehebu
ya Kikristo wasichague CCM, umefikiwa katika mkutano wa jukwaa hilo uliofanyika
katika ukumbi wa Baraza la Maaskofu, Kurasini jijini Dar es Salaam, Jumanne
wiki hii.
Mtoa taarifa wa amekiambia chanzo changu kuwa
maaskofu walifikia uamuzi huo baada ya kuchoshwa na walichoita, “kigeugeu cha
serikali katika kushughulikia Katiba Mpya na Mahakama ya Kadhi.”
Mkutano wa Maaskofu ulijadili kwa
kina suala la Katiba Pendekezwa na Mahakama ya Kadhi, pamoja na masuala
mengine, ikiwamo usalama wa nchi ulivyo kwa sasa na mustakabali wake.
Mwamvuli wa Jukwaa la Wakristo
Tanzania, ni jumuiko la pamoja la Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC),
Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) na Baraza la Makanisa ya Kipentekoste
Tanzania (CPCT).
Vyanzo vya taarifa kutoka ndani ya
mkutano vinamnukuu Askofu mmoja mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kulutheli
Tanzania (KKKT) akisema, kanisa limetuhumu serikali kushindwa kuchukua hatua
kutokomeza vitendo vya kigaidi, mauaji ya albino na uvunjifu wa amani.
Aidha, kanisa limetuhumu
serikali kutaka kuingiza nchi katika vita vya kidini kwa kitendo chake cha
kutaka kuruhusu kuwapo kwa Mahakama ya Kadhi na mahakama hiyo, kutambulika na
sheria za nchi.
“Katika hili la Mahakama ya Kadhi na
Katiba Pendekezwa, maaskofu walikuwa wakali sana. Kwa kweli, wametoa matamshi
ambayo hayajawahi kutolewa na viongozi wa kidini, tangu kanisa kuumbwa nchini,”
ameeleza kiongozi mmoja wa kidini aliyehudhuria mkutano huo.
Amesema, “Maaskofu wamekasirishwa na
kitendo cha Mizengo Pinda (waziri mkuu), kubeba suala la Mahakama ya Kadhi,
kama suala lake binafsi ili kutimiza adhima yake ya kutaka kuwa Rais.”
Akizungumzia Katika Pendekezwa, mtoa
taarifa anasema, maaskofu hawataki kura ya maoni ipigwe kwa kuwa wamejiridhisha
mchakato wa Katiba, umeligawa taifa na serikali imeshindwa kusimamia zoezi la
kura ya maoni.
Amesema, “katika kutilia mkazo hoja
hiyo, jukwaa la Wakristo likasisitiza waumini wake kutokipigia kura CCM.”
Katika tamko lake, Jukwaa
limesema, “…kwa kuwa chama tawala na serikali yake wameshindwa kusimamia
misingi iliyolea taifa kama serikali isiyo ya kidini na taifa lenye amani;
umoja na utulivu; linawaelekeza waumini wote na wenye mapenzi mema, wakati wa
uchaguzi mkuu ujao kufanya maamuzi yanayolitanguliza taifa badala ya kutanguliza
mazoea, mapokeo, itikadi na ushabiki wa chama fulani cha siasa.”
Chanzo cha Mwanahalisi.online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni