SERIKALI YASALIMU AMRI KWA WAANDISHI WA HABARI,YAKUBALI KUPELEKA MSWAADA BUN GENI,SOMA HAPA KUJUA
HATIMAYE serikali imekubali kuwasilisha bungeni miswaada miwili muhimu kwa sekta ya habari nchini. Anaandika Yusuf Aboud … (endelea).
Miswaada hiyo miwili itakayowasilishwa katika Mkutano wa Kumi na Tisa wa Bunge la Kumi, ni Muswada wa Sheria ya kupata habari wa mwaka 2015 –The Access to Information Bill (2015) na muswada wa sheria ya vyombo vya habari wa mwaka 2015 –The Media Services Bill (2015).
Rais Jakaya Kikwete aliahidi tangu Septemba 24, 2014, akiwa jijini London, kuwa sheria ya Uhuru wa kupata Habari ingepatikana kabla ya Februari mwaka huu.
Rais alitoa ahadi hiyo, alipokuwa mmoja wa wazungumzaji katika mkutano unaohusu “uwazi na ushirikiano kati ya serikali na jamii (Open Government Partnership-OGP).”
Akizungumzia muswaada huo, mwandishi wa habari mahiri nchini, Saed Kubenea amesema, muswaada huo umechelewa mno; kuwasilishwa kwa miswaada hiyo miwili kutakuwa hakuna maana ikiwa hakutaondolewa sheria kandamizi katika nchi.
“Uhuru wa Habari ni muhimu kwa wananch. Ni haki ya msingi ya raia kuwawezesha kufanya maamuzi yanayofaa kuhusu maisha yao. Muswaada huu utasaidia wananchi kufahamu serikali yao inafanya nini kwa niaba yao,” ameeleza Kubenea.
Miswaada mingine ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge hilo, ni pamoja na muswaada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na. 2) wa mwaka 2014 –The Written Laws (Miscellaneous Amendements) (No. 2) Bill, 2014].
Muswaada wa sheria mbalimbali, unalenga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi; muswaada ambao unakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa viongozi wa madhehebu ya kidini.
Aidha, kwa mujibu wa kanuni ya 81 (1) ya Kanuni za Bunge, katika mkutano huu, kunatarajiwa kuwasilishwa muswada mmoja binafsi.
Muswaada huo, utawasilishwa bungeni na John Mnyika, mbunge wa Chadema, katika jimbo la Ubungo.
Muswada unahusu Sheria ya Baraza la Vijana la Taifa wa Mwaka 2013 (The Nationa Youth Council Bill, 2013).
Hakuna maoni
Chapisha Maoni