BREAKING NEWS--DOKTA SLAA KUBULUZWA MAKAMANI,MAKADA WAKE,KAGENZE NAO PIA,KAMANDA KOVA ABWATA SOMA HAPA KUJUA
NA KAROLI VINSENT
JESHI la
Polsi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lipo katika hatua ya mwisho katika kukamilisha
ushahidi ili kumfikikisha mahakamani Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na
maendeleo Chadema Dokta Wilbroad Slaa pamoja na makada wa Chama hicho.
Akizungumza
na waandishi wa Habari mda huu Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Polisi Kanda
maalum Dar es Salaam Suleimani Kova ametaja sababu ya kumfikisha mahakani
katibu huyo wa Chadema na Makada wake inatokana na Vitendo vinavyodaiwa ni vya
kinyama alivyofanyiwa mlinzi wake vya kumteka,kumpiga na kumlazimisha kutaja
watu wanaomtuma kumuua Katibu mkuu wa Chadema.
Hivyo hivyo
Jeshi hilo la Polisi limesema kwa sasa linawashikilia makada watatu wa Chama
hicho kikuu cha upinzani nchini ambao ni Boniface Jacob miaka 32 mkazi wa
ubungo kisiwani ambae pia ni diwani wa kata ya Ubungo kupitia chama hicho.
Sambamba na
Hemed Ally Sabula miaka 48 mkazi wa Tandale kwa tumbo ambaye anadaiwa ni Afisa
Usalama wa chama hicho Taifa.
Mbali na hao
pia Kamishna Kova amemtaja Kada mwengine anayeshikiliwa kuwa ni Benson
Mramba,miaka 30,mkazi Tabata Kisukulu ambaye ni Afisa Utawala wa Chadema.
Kamishna
kova amebainisha kuwa Ushahidi wao utakapokamilika mafaili yao yatafikishwa kwa
Wakili wa Serikali ili hatua zichukuliwe.
Aidha,Akizungumzia sakata la Mlinzi
Kagenzi amesema kwa sasa wanamalizia kazi ya kukusanya ushahidi kutoka Chadema
ambao wanamtuhumu bwana Kagenzi ambaye anafanya ushirikiano na Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM bara Philip Mangula na Afisa Usalama wa
Taifa Mkoa wa Kinondoni kwa kuaandaa mpango wa kutaka kumuwekea sumu Dokta Slaa.
Kesi hiyo
kwa mala ya kwanza ilifika polisi tarehe 8 mwezi huu majira ya saa 11.jioni
katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kupitia kwa wakili wa Chadema
anayetambulika kwa jina la john Malya akiambana na mtuhumiwa Khalid Kagenzi
ambaye ni mkazi wa Tandale kwa tumbo ambapo Wakili huyo aliiambia polisi kwamba
alimleta mtuhumiwa baada ya kuagizwa na Dokta Slaa ili kutoa malalamiko kwa
niaba yake.
Ambapo
Katika maelezo yake anadai Wakili huyo kuwa
uongozi wa Chadema ulikuwa ulichukuwa hatua mbalimbali dhidi ya kugenzi
ikiwemo kumbana na kujilidhisha kuwa nahusika na mipango ya kimauaji.
Kwa mujibu
wa Kamishna kova anasema katika mahojiano wakabaini kunavitendo vya kinyama
ambavyo mlinzi huyo wa Dokta Slaa amefanyiwa na Makada wa Chadema baada ya
Jeshi hilo kumkuta akiwa na majeraha mbalimbali katika mwili wake.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni