IDARA YA UHAMIAJI YALIVAA GAZETI LA JAMHURI,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji na Msemaji wa idara ya Uhamiaji nchini Abbas Irovya Akizungumza na Waandishi wa Habari leo |
IDARA ya
Uhamiaji nchini imekanusha Habari iliyoandikwa na Gazeti la Jamhuri ambayo
Habari hiyo ilikuwa inawatuhumu viongozi
wa idara hiyo kuhusika katika biashara ya kusafirisha binadamu nchini.Anaripoti
KAROLI VINSENT.Endelea nayo.
Akikanusha Taarifa hiyo leo Jijini Dar
es Salaam wakati wa mkutano na Vyombo vya Habari.Naibu Kamishna wa Uhamiaji na
Msemaji wa idara ya Uhamiaji nchini Abbas Irovya amesema Idara hiyo inasikitika
na taarifa anayodai ni ya upotoshaji iliyoandikwa na Gazeti la Jamhiri toleo
namba 180 la tarehe 10-16 machi mwaka huu ambayo-
Iliandikwa makala kwenye ukrasa wa kwanza
ilikuwa na kichwa cha Habari “Uhamiaji waamua ‘Kuuza nchi”na katika ukrasa wa
tatu ikaandikwa tena “Uhamiaji wauza nchi”
Kamishna Irovya amesema katika makala
hiyo ya Habari kunamadai ambayo mwanadishi wa habari anawashutumu Viongozi wa idara ya Uhamiaji kuhusika na mtandao wa wafanya
biashara ya kusafirisha binadamu duniani kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa
nchini Pakistani.
“Napenda kuwafahamisha umma kuwa hakuna
mtandao wawafanya biashara kusafirisha binadamu kutoka Pakistani na hapa nchini
kama inavyodaiwa na Makala hiyo,na hivyo kusema kauli za maisha ya watanzania
yamo hatarini haina msingi kabisa”Amesema Kamishna Irovya.
Kamishna Irovya ameongeza kuwa kuhusu
madai yaliyotolewa na gazeti hilo kwamba kuna mtu anayejulikana kwa jina la
Ajaz Ahmed ambaye wanadai ni kiongozi wa mtandao wa Usafirishaji binadamu hapa
nchini na kwamba gazeti hilo linadai kwamba baada ya kuondoka nchini amerejea
kupitia mpaka wa namanga kuja kuendelea na biashara hiyo sio kweli.
“Huu ni uwongo mkubwa sana unaoadikwa
na Gazeti hili kwani huyo mtu wanayemtaja anayefahamika kwa jina Ajaz Ahmed
Muhammad raia wa Pakistani alishtakiwa kwa kesi ya kijihusisha ma ni biashara
ya binadamu (Kesi ya jinai na 176/2014)
na tarehe 28 oktoba mwaka 2014 na”
“Alikubali mashtaka yake na hivyo kuhukumiwa
miaka 10 kwenye Mahakama ya kisutu au kulipa faini milioni tano na laki tano na
tarehe hiyo alilipa na akapewa taarifa ya kuwa mtu asiyetakiwa hapa nchini
(Prohibited Immigrant Notice) namba 0050968,ambayo ilimtaka aondoke nchini ndani ya saa 24,na ndugu Ajaz aliondoka
nchini tarehe 29 oktoba kwa ndege ya shirika la ndege Qatar na ajawaikurudi
tena”ameongeza Kamishna Irovya.
Vilevile Kamishna irovya akawataka
waandishi wa Habari kuandika taarifa zenye ukweli na kuacha kuandika habari
zenye kupotosha umma.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni