UFISADI WA ESCROW WAMTESA PROF-TIBAIJUKA,KAFARA YAKE YAMFANYA AWAANGUKIE WANANCHI WAKE SOMA HAPA KUJUA
Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akiwa kwenye Baraza la Sekretarieti ya Maadili ya Watumishi wa Umma |
PROFESA Anna
Tibaijuka-Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), ameanza ziara jimboni inayotafsiriwa
kama ya “kujitakasa” kutokana na kashfa ya mgawo wa sh. bilioni 1.6 za Akaunti
ya Tegeta Escrow inayomkabili. Anaadika Edson Kamukara … (endelea).
Hatua hiyo inakuja baada ya mwanasiasa
huyo kujaribu bila mafanikio kujitetea kwenye vyombo vya habari vya ndani na
nje ya nchi ili asivuliwe wadhifa wake wa uwaziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi.
Prof.
Tibaijuka amevuliwa uwazi pamoja na kusimamishwa kwa muda ujumbe wa Kamati Kuu
ya CCM kwa kosa la kukiuka maadili ya viongozi wa utumishi wa umma akidaiwa
kupokea sh. bilioni 1.6 kutoka kwa mmoja wa wabia wa Kampuni ya kufua umeme ya
Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari
kutoka Muleba, Machi 13 mwaka huu, Prof. Tibaijuka alilazimika kuitisha kikao
“kizito” nyumbani kwake ili kupata tathmini ya hali yake kisiasa jimboni baada
ya kukumbwa na kashfa hiyo.
Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na washirika
wake wa karibu wakiwemo wanafamilia, viongozi wa CCM na wadau mbalimbali,
inaelezwa kuwa mbunge huyo aliambiwa hali yake kisiasa jimboni ni tete tofauti
na anavyofarijiwa na wasaidizi wake.
“Miongoni mwa waliomweleza ukweli ni
mshirika wake wa karibu (anatajwa), huyu alimwambia namna ambavyo watendaji
wake wameshindwa kuwa na mahusiano mema na wananchi na hivyo kumfanya achukiwe.
“Alichoshauriwa ni kuanza ziara ya
haraka kutembelea kata zote huku akitekeleza ahadi alizotoa wakati wa kampeni
za mwaka 2010 na vile vile kuendelea kutoa ahadi mpya ambazo zitatekelezwa
iwapo atachaguliwa tena,”anaeleza mtoa taarifa.
Katika ziara hiyo
ambayo imeanza Machi 15 mwaka huu, katika Kijiji cha Kiholele Kata ya Bureza,
Prof. Tibaijuka anadaiwa kupata wakati mgumu wa kueleza jinsi alivyotekeleza
ahadi zake, hali iliyomlazimu “kumwaga” fedha kutuliza upepo.
Chanzo changu kimedokezwa kuwa mbunge
huyo kabla ya kukumbwa na kashfa ya Escrow amekuwa akitoa michango ya maendeleo
au kuhadi misiba kwa sh. 100,000 kupitia kwa wasaidizi wake lakini sasa
anafanya hivyo mwenyewe tena kwa kuongeza dau.
“Tangu sakata hili la Escrow ameongeza
dau, anatoa sh. 150,000 kwa kila tukio na kazi hiyo imeanza juzi katika Kata ya
Magata Karutanga kwenye msiba wa (anatajwa) na baada ya hapo alielekea katika
msiba mwingine kata ya Karambi,”kinasema chanzo kingine.
Taarifa hizo zinaongeza kuwa akiwa
katika Kata ya Gwanseli, Tibaijuka ambaye kwa siku nzima ya jana hakupatikana
kufafanua madai hayo, anadaiwa kutoa sh. 250,000 kwa vijana aliowakuta
wakicheza mpira kwenye kitongoji cha Kaina.
Akiwa Kata ya Bureza, Tibaiujuka
alibanwa na wapiga kura aeleze kwanini hajatekeleza ahadi yake ya kuijenga
barabara hiyo ambayo hata siku alipotembelea hapo alishindwa kufika kwa gari
kutokana na kuharibiwa vibaya na mvua.
Kama alivyofanya kwenye maeneo mengine,
pia Tibaijuka aliwaahidi wananchi hao kuwa atachangia sh. milioni 2 kwa ajili
ya ukarabati wa barabara hiyo na kisha akatoa ada ya 100,000 kwa wanafunzi
wawili (kila mmoja 50,000) na kuchangia sh. 100,000 kwa kikundi cha akina mama.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, Prof.
Tibaijuka alijikuta akilazimika kutengua ahadi yake ya kujenga kwa kiwango cha
lami barabara kati ya Muleba hadi Hospitali Teule ya Wilaya ya Rubya yenye
urefu wa km 13.
Ahadi hiyo aliitoa mwaka juzi wakati wa
ziara ya Rais Jakaya Kikwete, akisema kuwa serikali imekubali kuijinga barabara
hiyo kwa kiwango cha lami kabla hajamaliza ubunge wake.
Lakini juzi alipobanwa na wapigakura
wake, Prof. Tibaijuka amesema ahadi hiyo haitawezekana kutekelezeka kwa muda
uliyobakia kwa vile hakujua kama kiasi cha fedha kinachohitajika zaidi ya sh.
bilioni 21 kingekuwa kikubwa hivyo
Chanzo ni
Mwanahalisi.Online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni