HABARI KUBWA LEO-MAJANGA KWA ZITTO,CHAMA CHAKE KUKWAA KISIKI TENA
Katibu Mkuu wa ACT-Tanzania, Samson Mwigamba akionesha katiba ya chama hicho |
HATIMA ya Chama cha
Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), iko mikononi mwa Jaji
Mwandambo wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. Anaandika
Mwandishi Wetu … (endelea).
Hii inatokana na Lucas Kadawi Limbu,
kufungua shauri la madai Na. 17 la mwaka 2015, dhidi ya Samson Mwigamba na
mawakala wake.
Uchaguzi mkuu wa ACT-Tanzania
umepangwa kufanyika Machi 29 mwaka huu, lakini Limbu ambaye anajitambulisha
kama Mwenyekiti “halali” wa chama hicho, amefungua shauri kujiridhisha kama
Mwigamba na wenzake wako madarakani kwa msaada wa Rais Jakaya Kikwete kama
wanavyotamba au la.
Anasema “nataka kujiridhisha kwa Msajili
wa Vyama vya Siasa kama kweli Samson Mwigamba (Katibu Mkuu), Peter Mwambaja
(mweka hazina) na Masanga M. Masanga (Mwenezi), wanasaidiwa na Rais Kikwete
kuendelea kubaki madarakani wakati ni kinyume cha katiba ya ACT-Tanzania”.
Kwa mujibu wa Limbu, shauri hilo ambalo
limefunguliwa tangu tarehe 30 Januari 2015, limetajwa leo na kuahirishwa
hadi tarehe 15 Aprili mwaka huu.
Alipoulizwa kama haoni
kwa tarehe hiyo tayari ACT-Tanzania itakuwa imemaliza uchaguzi wake, Limbu
amesema, “sisi hatukutaka kuweka pingamizi kuzuia u chaguzi huo ambao sio halali,
isipokuwa tumemwachia Jaji atumie busara yake”.
Limbu anasisitiza kwamba, hata Jaji
Mwandambo akiacha uchaguzi huo ufanyike, bado hatua hiyo itakuwa sawa na kazi
bure kwani itakapobainika huko mbele kuwa Mwigamba hawakuwa viongozi halali,
hawataweza kulalamika kwamba walipoteza fedha.
“Mimi ndiye mwenyekiti halali wa
ACT-Tanzania, hakuna mtu wala kikao kilichokaa na kuniondoa, hizo mbwembwe za
msajili wa vyama kwamba anawatambua Mwigamba na wenzake ni za kuwaridhisha tu.
Amefafanua kuwa inashangaza kuona msajili wa
vyama anadai kumtambua Mwigamba na wenzake ilhali walikwitangaza kujiuzulu
tangu tarehe 5 Desemba 2014 katika Kamati Kuu.
“Sasa watu hao hao wanawezaje kuitisha
kikao cha Sekretarieti tarehe 23 Desemba 2014 na ‘kujipachika’ madaraka ya
kunisimamisha halafu eti tarehe 10 Februari 2015, msajili anatoa barua ya
kutambua maamuzi yao.
“Yaani tarehe 16
Februari 2015, msajili ametoa barua nyingine ya kutangaza kuniengua kwenye
Baraza la Vyama vya siasa. Hapa ndipo nataka kufahamu nani yuko nyuma ya
ufisadi huu. ACT walikaa lini kunifukuza na kupelekea taarifa kwa msajili,”
anahoji.
Limbu ambaye anashirikiana na Leopord
Mahona na Greson Nyakarungu katika shauri lake, amesema kuwa uchaguzi
ulioitishwa na wakina Mwigamba sio halali kwa mujibu wa katiba.
ACT-Tanzania ambayo iko mbioni kumpokea
Zitto Kabwe ambaye ametimuliwa uanachama na chama chake cha Chadema, imekuwa
kwenye msuguano wa uongozi baina ya waanzilishi na wananchama waliojiunga
baadaye.
Desemba 31, mwaka
jana, Kamati Maalum ya ACT-Tanzania, ilipitisha kwa pamoja azimio la kuwafukuza
kutoka ndani ya chama hicho, viongozi wake watatu wajuu, Samson Mwigamba, Prof.
Kitila Mkumbo, mjumbe wa kamati kuu (CC) na Shaban Mambo, Makamu mwenyekiti
Bara, huku Zitto Kabwe akitajwa kuwa sababu ya kutimuliwa kwao.
Akisoma azimio la kufukuzwa viongozi hao,
Mwenyekiti Limbu alisema, Prof. Kitila na Mwigamba wamevuliwa uwanachama
kwa kosa la kuanzisha chama kipya ndani ya chama cha sasa.
Limbu amesema, Kitila na Mwigamba
wamethibitika kupeleka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa katiba mpya ya ACT, kisha
kuisambaza mikoani, kinyume na katiba iliyopo ya chama hicho; kuchapisha
bendera mpya, kadi na nembo.
Aidha, Prof. Kitila na Mwigamba
wanatuhumiwa kupokea fedha kutoka kusikukojulikana, ikiwa ni sehemu ya
mabilioni ya shilingi yaliyokwapuliwa kutoka Akaunti ya Escrow.
Vilevile, Prof. Kitila na Mwigamba
wamefukuzwa uwanachama wa chama hicho kwa kukiri kukiingiza katika mkataba wa
uendeshaji na kampuni ya kigeni kutoka Senegal na bila chama kufahamishwa.
Taarifa zinasema, mbali na makosa hayo,
Prof. Kitila na Mwigamba wamefukuzwa katika chama, kutokana na kushiriki
maandalizi ya kufanya “mapinduzi” ya kumwondoa mwenyekiti wa sasa Limbu ili
Zitto Kabwe aweze kushika usukani wa chama hicho.
Chanzo ni
Mwanahalisi.online
Post Comment
Hakuna maoni
Chapisha Maoni