HABARI KUBWA -USALAMA WA TAIFA WATETEWA,KAMISHNA KOVA AWARUDIA CHADEMA NI MIPANGO YA KUMUUA DK SLAA,SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Kamishna wa Kanda Maalum ya Polis Mkoa wa Dar es Salaa Suleiman Kova\ Akizungumza na Waandishi wa Habari mda huu jijini Dar |
JESHI la
Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limekanusha kuhusika kwa Idara Usalama wa Taifa katika mipango ambayo
inaidaiwa ya kutaka kumuua Katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
Chadema Dokta Wilbroad Slaa.Anaripoti KAROLI VINSENT.Endelea nayo
Kauli ya jeshi la polisi kanda hiyo ni
kama inakuwa inamjibu Mjumbe wa kamati kuu ya chadema CC,Mabere Marandu ambaye
katika taarifa yake kwa vyombo vya Habari alimtuhumu Naibu mkuu wa idara ya
Usalama mkoa wa Kinondoni Elisifa Ngowi kuandaa mipango miovu kwa dokta Slaa
akishirikiana na Mlinzi wa Katibu huyo-
Bwana Khalid Kagenzi pamoja na Makumu mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi CCM Tanzania Bara,Philip Mangula.
Akikanusha taarifa hizo leo Jijini Dar
es Salaam,Kamishna wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam,Suleiman Kova wakati
na mkutano na vyombo vya Habari amesema Jeshi hilo limefanya uchunguzi wakina
ikiwemo kuchukua taarifa upande wa chama cha Chadema na Mlinzi wa Dokta Slaa na
kubaini hakuna ukweli idara ya Usalama wa Taifa kuhusika.
“Kiukweli bado tunaendela na uchunguzi
ikiwemo kuwahoji watu wote wanaotuhumiwa tumebaini kwa dhati kabisa hakuna mtu
yeyote wa usalama wa Taifa kuhusika katika mipango ya kumdhulu Dokta Slaa na
tena nomba iwe hivyo”Amesema Kamishna Kova.
Kamishna Kova,ameongeza kuwa kwa sasa bado
wanaendelea na uchunguzi wa suala hilo na uchunguzi ukikamilika watafawakisha
watu mahakamani bila hata kumwogopa mtu yeyote.
“Mbona nyie waandishi wa habari mnaangali
upande wa usalama mbona amtuhoji kama tumemuhoji nani upande wa Chadema lakini
ukweli ni kwamba tunaendelea na uchanguzi ikiwemo mahojiano ya kina kati ya
watuhumiwa wote wale wanao tuhumiwa na chadema pamoja na Mlinzi wa Dokta Slaa
bwana Kagenzi”
“Nawahakikishia uchanguzi ukikamilika
lazima wafikishwe mahakamani na sisi hatutanii”Ameongeza Kamishna Kova.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo kanda
Maalum ya Dar es Salaam linawashikiria watu wawili waojiita ni viongozi wa watu
waliopata mafunzo ya mgambo kwa kosa la kuratibu na kuongoza vikao vya
uchochezi vya mgambo dhidi ya serikali.
Kwa,mujibu wa Kamishna Koma amewataja
watuhumiwa kwa majina ni Mathias lubega
miaka 43,mkazi wa bunju ambaye amekamatwa maeneo ya Mission pup huko mbagala
mkoa wa polisi Temeke.
Wa pili ni Mohamed Ally miaka 38 naye pia ni mkazi wa Mbagala .
Mbali na kuwakamata watuhumiwa hao kamishna
Kova alithibitisha kuwa jeshi hilo katika msako wake mkali limefanikiwa
kukamatwa kwa noti bandia za dolla za kimarekani azipatazo 426 ambazo ni noti
36 ni za dolla 100 na noti 390 za dolla 50.
Kamishna kova pia aliwataja kwa majina
watuhumiwa ambao pesa hizo zilikutwa kwao ni Ramadhani Mhambo miaka 34,mkazi wa
Mwanayamala jijini hapa,Eliazr Jackob Nkurarumi na Juma Mohamed mrundi miaka 25
ambaye ni mlinzi wa Colombia Hoteli.
Mbali na watuhumiwa hao Kamishna Kova
aliwataja watuhumiwa wengine ni Rajabu Nassor vmiaka 30 ambaye ni fundi simu,Mkazi
wa mwananyamala kwa sindano ambapo wote walipkuwa kwenye makazi yao walikutwa
na fedha hizo bandia.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni