KANISA KATOLIKI LAGAWANYIKA,KAULI YA ASKOFU KILAINI NA PENGO YADUWAZA WAAMINI WAO.SOMA HAPA KUJUA
ASKOFU Msaidizi wa Jimbo la Bukoba, (pichani)Methodius
Kilaini, amekana kujiengua na viongozi wenzake wa madhehebu ya Kikristo
wanaosisitiza waumini wao kupigia kura ya hapana Katiba Pendekezwa. Anaandika Saed Kubenea … (endelea).
Akiandika kwa njia ya ujumbe mfupi wa
simu ya mkononi (sms), kwenda kwa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki
(TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa, Askofu Kilaini amekana madai kuwa yeye
amepingana na viongozi wenzake wa madhehebu ya Kikristo. Amesema,
“Baba pole na kazi na hongera kwa tamko lako. Uhuru wananisingizia eti niko
nao. Wapumbavu.”
Alilazimika kutoa
ufafanuzi huo baada ya gazeti linalomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) la
Uhuru la Alhamisi 19 Machi 2015, kudai kuwa Askofu Kilaini ameungana na Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, kupinga msimamo wa maaskofu.
Amesema,
gazeti linalotumika na CCM kufanyia propaganda lilidai kuwa Askofu Kilaini
ameungana na Kardinali Pengo kuwakana viongozi wenzake wa madhehebu ya Kikristo
waliotaka waumini wao kupigia kura ya hapana Katiba Pendekezwa.
Akifungua mafungo ya
Wanawake Wakatoliki Tanzani, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Pengo
alisema, “..sisi maaskofu hatuna mamlaka ya kulazimisha wakristo au waamini pamoja
na watu wengine… kuwalazimisha watende kitu kinyume cha dhamiri yao.”
Kardinali Pengo
alikuwa akizungumzia matamko mawili, ya Jukwaa la Wakristu na la Baraza la
Maaskofu Tanzania.
Hata hivyo,
Kardinali Pengo amekiri kuwa viongozi waliotoa matamko hayo, ni watu wakubwa
sana; wamekabidiwa madaraka makubwa katika kanisa na hawawezi kupuuzwa kwa
sababu matamko yao wameyatoa baada ya tafakari kubwa.
Amesema, “Jambo ambalo ningependa kila moja
wetu atambue ni hili; kwamba matamko yote mawili yanaashiria mgawanyiko wa
taifa letu, kati ya wakrtisto na wasiokuwa wakristu.”
Amesema, “Lazima
tulitambue na tutambue kwamba matamko haya yanaweka Jumuiya ya Wakristu dhidi
ya serikali ya nchi yetu ya Tanzania. Haya mambo mawili lazima tuyatambue
wakati tunasoma matamko haya…”
“…Nikiwa katika
hali hii ta ukamilifu nililetewa nakala hii iliyopo hapa mbele yangu,
nikaulizwa je, isomwe katika makanisa ya maparokia zote katika Jimbo Kuu la Dar
es salaam? Nikasema mimi ni nani kupinga jambo ambalo limeshatamkwa na maaskofu
wote. Kwa nini nizuie, hata nikizuia yamechapwa katika magazeti na yatachapwa
katika magazeti. Kwa nini nizuie waamini wakatoliki katika parokia zao wasijue
haya yaliyoandikwa, sina sababu.”
Kardinali Pengo amesema, “Lakini
nililonalo ambalo ni muhimu kwangu kama mchungaji ni kutoa maoni yangu mbele
yenu kuhusu barua zote hizi mbili. Barua zote mbili kama nilivyosema
zimetengenezwa kutokana na umakini wa hali ya juu, lakini sisi maaskofu hatuna
mamlaka ya kulazimisha wakristo…”
Amesema, “Tungekuwa na
mamlaka hayo tukawa tumeyapokea kutoka kwa Mwenyezi Mungu, tungemwuliza
mwenyezi Mungu kwa nini hujatumia mamlaka hayo watu wanaendelea kutenda
madhambi na wewe unawatazama.”
Lakini kwa sauti njia ya unyenyekevu, Askofu Kilaini, ambaye
amewekwa Wakfu na Kardinali Agnelo Rossi mwaka 2000 amesema, “…Uhuru
wamenisingizia. Sina mamlaka ya kupingana na kanisa na wala ndani ya moyo wangu
sijawahi kuwa na dhamira ya aina hiyo.”
Askofu Kilani
alizaliwa Katoma, Bukoba tarehe 30 Machi 1948 na kutunukiwa shahada ya pili ya
Teolojia huko Roma. Aliwahi kuwa katibu mkuu wa TEC.
Madhehebu ya Kikristo nchini yametaka serikali kusitisha mpango
wake wa kuwasilisha bungeni musaadwa wa marekebisho ya Sheria Na. 2 juu ya
Tamko la Sheria ya Kiislam ya mwaka 1964.
Taarifa iliyotolewa na
Jukwaa hilo hivi karibuni, imesema Muswada huo unaolenga kuanzishwa kwa
Mahakama ya Kadhi utasabisha kuvunjika kwa misingi ya taifa hili na kuibua
hisia za kibaguzi.
“Mapendekezo
ya kurekebisha Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu ni mapendekezo makubwa
yatakayokuwa na athari kubwa na nzito; kwani yanahoji msingi wa dola ya
Tanzania kama dola isiyokuwa ya kidini,” wameeleza maaskofu.
Tamko la madhehebu
ya kidini limesainiwa na Askofu Dk. Alex Malasusa, Askofu Ngalalekumtwa na
Askofu Daniel Awet kutoka CPCT.
Kwa mujibu wa tamko
hilo, Mahakama za Kadhi, pamoja na Mahakama za Wenyeji (Native Courts),
zilizokuwepo wakati wa ukoloni zilifutwa na Sheria ya Mahakama za Mahakimu
(Magistrates Courts Act) ya mwaka 1963.
Wamesema, “Tangu
wakati huo, mahakama hizi hazipo na hazitambuliwi na sheria yoyote. Hivyo,
mapendekezo ya muswada huu yakipitishwa yatakuwa yanaanzisha mahakama hizo.”
Chanzo ni
Mwanahalisi.online
Hakuna maoni
Chapisha Maoni