KASHIFA ZA ESCROW, EPA,RADA ZIMETIA HASARA TAIFA BILIONI 250-LHRC, NI NDANI YA UONGOIZ WA JK
Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba, wakati akitoa taarifa juu ya mwenendo na hatua za kisheria kwa viongozi wa umma wanaokiuka maadili.Katikati ni Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na kulia ni Ofisa Programu Dawati la Waangalizi Watendaji wa Serikali wa LHRC, Hussein Sengu. |
Hatimaye Kituo cha sheria na haki za binadamu nchini tanzania (LHRC) kimevunja ukimya kwa kujitokeza hadharani kwa mara ya kwanza na kuitaka serikali kuwachukulia hatua za kinidhamu maofisa wa serikali wanaotoa kauli za kikebehi,dharau na jeuri kwa watanzania mara tu wanapotenda makosa yao
Akizungumza na waandishi wahabari ofisini kwake Mkurugenzi wa utetezi na maboresho wa kituo cha Sheria na haki za binadamu (LHRC)mwanasheria Harold Sungusia amesema kwa takribani muongo mmoja sasa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa viongozi wa umma, kwa viongozi wetu kutumia vibaya rasilimali zetu pamoja na viongozi hao kujilimbikizia fedha nyingi na mali kinyume cha sheria
Amesema ili kurejesha nidhamu kwa viongozi hao, hakuna budi sasa kwa Serikali ikaanza kuwachukulia hatua za kinidhamu hawa wa sasa ili wawe mfano kwa vizazi vijavyo na taifa kwa ujumla
Sungusia anasema kwa kipindi cha miaka tisa pekee, tayari taifa limeingia katika kashfa nzito nne ambazo limezighalimu taifa jumla ya Tsh bilion 250 ambazo ni sawa na wastani wa bajeti ya taifa 20% ya kila mwaka
Akitaja kashifa hizo ambazo zimepelekea taifa kuingia hasara ya mabilini ya shilingi, Sungusia amesema ni pamoja na ile ya ununuzi wa Rada iliyotumika kutoka katika kampuni ya BAE system ya Uingeleza, Wizi wa mabilioni katika akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) ndani ya benki kuu (BOT), Mkataba usio na tija kwa taifa wa kampuni ya Richmond na kashfa ya babilioni ya pesa waliogaiwa viongozi wa juu na mfanyabiashara kutoka kwenye akaunti ya Tegeta Escrow
Sungusia ameendelea kusema kuwa kumekuwa na kauli za dharau na kejeli
ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wananchi kutoka kwa viongozi wao pale ambapo
wananchi wanapohoji mambo ya msingi na kumekuwa hakuna hatua zozote ambazo zimekuwa
zikichukuliwa kwa viongozi hao jambo ambalo amesema kuwalinawapa kiburi kuwa
hakuna yoyote anayeweza kuhoji.
Akitolea mfano wa baadhi ya kauli ambazo zimewahi
kutolewa na viongozi wa Tanzania amesema kuwa moja ya kauli ya kuudhi
iliyotolewa katika sakata la pesa za ESCROW ambayo ilitolewa na aliyekuwa
waziri wa ardhi ANNA TIBAIJUKA ambapo wakati akihojiwa na baraza la maadili alisema kuwa “HIYO MILLION KUMI SI
NI PESA YA MBOGA TU”kauli ambayo amesema kuwa inaudhi ukizingatia kuwa
watanzania wengi wanaishi chini ya dola moja.
Kauli nyingine zilizotolewa na viongozi mbalimbali
wakati wakijitetea katika ukwapuaji wa fedha za ESCROW ni pamoja na “Sikumwomba
james rugemalila aniwekee hela,na sijui kwa nini aliniwekea hela hizo,hata alivyoniambia
nifungue account bank ya mkombozi ili aniwekee fedha hizo sikumuuliza fedha
hizo ni za nini”
Kauli nyingine ni ile inayosema “nina account nyingi
na za nje ya nchi ningetaka ningemwambia aziweke fedha acount za huko”.
Amesema kuwa kauli hizo zilizotolewa katika sakata
la kuwahoji wahusika wa ukwapuaji wa fedha za ESCROW ni mwendelezo wa kauli
ambazo zimewahi kutolewa na viongozi kipindi cha nyuma kama kauli aliyowahi
kuitoa waziri CHENGE KUWA “hivi ni vijisent tu”na ile ambayo aliitoa waziri MAGUFULI
ya kuwataka wananchi wa kigamboni kama watashindwa kulipa mia mbili ya kuvuka
na panton bora waogelee kauli ambayo iliwaacha baadhi ya watanzania midomo wazi
kwa kusikia kauli kama hivyo kwa kiongozi waliyemchagua.
Amesema kuwa kwa kauli hizo ni wazi kuwa Tanzania
bado ina tatizo kubwa katika katika swala la uongozi na uwajibikaji wa viongozi
katika mfumo mzima wanchi.
Aidha amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto hii
ya viongozi wa Tanzania ni lazima sheria ya maadili ya viongozi wa umma
itekelezwe kama ilivyoanishwa na secretarieti ya maadili ya viongozi wa
umma,ikiwa ni pamoja na viongozi kuwajibishwa kwa kauli zao zenye kuonyesha
dharau kwa wananchi wa Tanzania.
Katika hatua nyingine bwana sungusia amesema kuwa
ikiwa Tanzania inaelekea katika mchakato wa kupata katiba mpya lakini bado
katiba iliyopendekezwa kwa ajili ya kupigiwa kura haijashinikiza uwepo wa uwajibikaji
kwa viongozi watakaochaguliwa kwa ajili ya kuwatumikia watanzania hivyo bado
katiba ijayo haiwezi kuwa dawa ya tatizo hilo nchini.
Kituo cha sheria kinapendekeza viongozi wote wawe chini ya sheria ya nchi kwa kuheshimu katiba harali ya taifa hususani ibara ya 132 na hap watakuwa wanaheshimu mamlaka ya sekritariet ya maadili.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni