ZITTO KABWE "NANG'ATUKA RASMI NIMEWAKOSEA ---- SOMA HAPA KUJUA,"
Zitto kabwe akitoka Bungeni jana baada ya kuwaaga wabunge wenzanke |
.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe
amewaaga rasmi wabunge baada ya kuvuliwa uanachama wa Chadema na kuahidi kuwa
“Mungu akipenda” atakuwa tena ndani ya chombo hicho cha kutunga sheria Novemba.
“Ni uamuzi mgumu ambao imebidi niukubali kwa matakwa ya chama,”
alisema Zitto alipopewa nafasi 3:14 muda mfupi kabla ya Bunge kumaliza shughuli
zake za jana.
Tulifurahi
pamoja, tulilia pamoja, na tulicheka pamoja. Naondoka na Mungu akipenda
tutakutana tena tutaonana Novemba,” aliongeza mbunge huyo ambaye alisifu kuwa
sehemu ya Bunge la Tisa ambalo alisema lilijenga misingi ya chombo hicho kuwa
na meno ya kuisimamia Serikali.
Mwanasheria wa
Chadema, Tundu Lissu alitangaza machi 10 mwaka huu kuwa Zitto amejivua rasmi
uanachama kutokana na kitendo chake cha kufungua kesi mahakamani kutaka katibu
mkuu wa Chadema ampe nyaraka za mwenendo wa vikao vya Kamati Kuu vilivyomvua
madaraka yote, kitu ambacho ni kinyume cha Katiba ya chama hicho kikuu cha
upinzani.
Lissu alitoa
tamko hilo saa chache baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali shauri la Zitto
kutokana na kutofuata taratibu zinazotakiwa kulifungua mahakamani.
Mwenyekiti wa
Bunge, Mussa Azzan Zungu alieleza kusikitishwa na uamuzi huo wa Zitto, akisema
anawaacha wabunge wenzake katika kipindi kigumu.
“Ni simanzi kubwa
kutuacha peke yetu katika kipindi hiki kigumu. Ushauri wako tutaukumbuka.
Umetambulika kimataifa na kitaifa utatambulika pia,” alisema Zungu.
Zitto,
ambaye alikuwa pia mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali,
alijipatia umaarufu wakati wa Bunge la Tisa kutokana na uwezo wake wa kujenga
hoja, hasa kwenye masuala ya mikataba ya madini.
Chanzo ni Gazeti la Mwananchi
Hakuna maoni
Chapisha Maoni