ZITTO KABWE AIBUKA NA BOMU JINGINE,SASA AUNGANA NA MBOWE KWENYE SAKATA LA UJENZI WA BOMBA LA GESI,SOMA HAPA KUJUA
pichani ni Zitto Kabwe picha na Maktaba |
Na
Fredy Azzah, Dar es
Salaam
Salaam
MWENYEKITI wa
Kamati ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC),
Zitto Kabwe, ameibuka tena na utata
wa Sh bilioni 821
ambazo Serikali ya Tanzania
imelieleza Shirika
la Fedha la Kimataifa (IMF),
kwamba imezitumia katika mradi wa
ujenzi wa
bomba la gesi
kutoka Mtwara kwenda Dar es
Salaam.
Mradi huo unaogharimu dola za
Marekani bilioni
1.55, kati yake
asilimia 95 ni mkopo wa masharti
nafuu kutoka Benki
ya Exim ya China na asilimia 5
ni fedha zitakazotolewa
na Serikali ya Tanzania.
Zitto ameibuka na
utata huo zikiwa zimepita siku
chache tangu
alipoonyesha wasiwasi juu ya
matumizi makubwa ya
fedha kwenye mradi huo
mwanzoni mwa mwezi
huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es
Salaam mwishoni mwa
wiki, Zitto alisema ripoti ya
Shirika la
Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC),
iliyowasilishwa kwa
kamati yake Novemba 3,
mwaka jana,
inaonyesha kuwa fedha ambazo
Tanzania ilikuwa
imetoa ni dola za Marekani 31.3.
“Fedha ambazo Serikali
imeahidi kutoa ni dola za
Marekani 61.4,
ambazo tayari ilishatoa ni 31.3,
lakini barua ya
Tanzania (Letter of Intent) kwenda
IMF, inasema
Serikali kwa mwaka wa fedha
ulioishia Juni
mwaka 2014, ilitumia dola za
Marekani milioni
464 (Sh bilioni 821), huu ni utata,
inabidi tupate
majibu.
“Hata kwa hizi fedha za kutoka
Exim Bank ya China
ni mkopo ambao
unatakiwa ulipwe kati ya 2020
hadi 2040, sasa
inakuwaje tena Serikali inaonekana
imezitumia fedha
hizo kabla hata ya muda wa
kulipa mkopo
haujafika?” alihoji Zitto.
Akifafanua kuhusu barua hiyo,
Gavana wa Benki
Kuu ya Tanzania
(BoT), Profesa Beno Ndulu, alisema
mradi huo
unagharimu dola za Marekani bilioni
1.25 ambazo
asilimia 95 ni mkopo wa masharti
nafuu kutoka Benki
ya Exim ya China.
Alisema dola za
Marekani milioni 464 ambazo
zimeelezwa kwenye
barua hiyo ya IMF ni sehemu
ya mkopo huo wa
Benki ya Exim.
“Ile dola milioni 464 ni
disbursement (malipo) ya
Exim ya China,
mkopo wote ni dola za Marekani
bilioni 1.25, kuna
namna tatu ya kuripoti madeni,
namna ya kwanza,
mwaka ule tulivyokubaliana
inakuwa ni
commitment, kwamba mkopo ni dola
bilioni 1.25, wale
wakasema fedha ni hizo na
zitatumika kulipa
ujenzi wa bomba, lakini hawatoi
cash, wanalipa
makandarasi, wanalipa shughuli za
ujenzi.
“Sasa disbursement ya ule mkopo
inafanyika kadiri
utekelezaji
unavyokwenda, kwa hiyo ile dola
milioni 464 maana
yake ni kiasi kilichotolewa
mwaka huo wa fedha
2013/14 kwa makandarasi
katika shughuli ya
kujenga huo mradi, siyo
kwamba fedha
inatolewa inakuja hapa sisi ndiyo
tuwalipe
makandarasi, inatolewa moja kwa moja
kulingana na kazi
iliyofanyika, benki hiyo inatoa
hiyo fedha kwa
niaba yetu.
“Kwa kuwa ule mradi hautekelezeki
kwa mwaka
mmoja tu, ni wa
karibu miaka miwili, kadiri
wanavyotekeleza
ndivyo wanavyolipwa, kwa mikopo
mingine wewe
unapewa hela kisha unawalipa
makandarasi, lakini
hii wanalipa wenyewe,
wanalipa kwa niaba
yako, hii itaenda hadi fedha
hiyo yote ya mkopo
iishe,” alisema Profesa Ndulu.
Akizungumza na
Chanzo changu jana, msimamizi wa
mradi huo kutoka
TPDC, Mhandisi Kapuulya
Musomba, alisema
hadi sasa Serikali ya Tanzania
imeshalipa asilimia
tano ya fedha hizo ambazo
ilipaswa kuzitoa.
Mhandisi Musomba alisema sehemu
ya fedha hizo
ni dola za Marekani
milioni 31.3 zilizotumika
kununua mashine
(compressor) inayotumika
Songosongo.
Alisema fedha
nyingine ni zaidi ya Sh bilioni 20
zilizotumika kwa
kufidia watu waliopisha mradi
huo na vitu vingine.
“Kwa sasa hivi hapa
sina takwimu zozote, lakini
ninachoweza
kukwambia ni kwamba ukijumlisha
mambo yote, hiyo
asilimia tano ya Serikali ni kama
dola za Marekani
94, na zote zilishatoka,” alisema.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni