CHUO KIKUU HURIA CHAZIDI KULETA MAPINDUZI YA ELIMU NCHINI,SHUHUDIA WALICHOKIFANYA
Makamu Mkuu wa chuo kikuu Huria cha Tanzania Prof Tolly Mbwette akifungua mafunzo kwa ajili ya wasichana yanayoendeshwa na chuo kikuu huria na shirika kutoka Canada linaloitwa Nafasi Opportunity Society (NOS).Ushirikiano huo umebobea kwenye kusaidia wasichana ambao hawajapata nafasi ya kupata mafunzo ya ufundi,mawasiliano na ujuzi wa biashara ili kuboresha nafasi zaidi za kujiajiri na kujenga uwezo wa kujiamini.Programu iyo itashirikisha pia VETA na Golden Touch Beauty College katika kutoa mafunzo ya utengenezaji wa nywele kwa kutumia utaalamu wa ndani.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiwahutubia wasichana waliokatika programu ya mafunzo inayoendeshwa kwa ubia kati ya Chuo Kikuu Huria na shirika kutoka Canada,Nafasi Opportunity Society(NOS).Prof Elisante alikazia zaidi kwa wasichana hao kuuza thamani na sio hujuzi walionao na kuzitumia changamoto walizonazo kuwa fursa.
Naibu Katibu Mkuu Prof Elisante Ole Gabriel akimtambulisha Afisa Maendeleo ya Vijana Bi.Caroline Malima kwa wasichana walio kwenye Programu ya mafunzo na kuwataka wawasiliane nae ili waujue mfuko wa maendeleo ya Vijana ambao ni fursa nzuri ya kujipatia mikopo katika vikundi ili kujianzishia miradi itakayowawezesha kujiajiri na kuboresha maisha yao.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa tatu kutoka Kulia) akifurahi jambo katika uzinduzi wa mafunzo ya wasichana yaliyojikita katika mafunzo ya ufundi,mawasiliano na ujuzi wa kibiashara.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa mafunzo kutoka VETA Bi.Leah Lukindo,anaefuata ni makamu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwette.
Uongozi wa Chuo Kikuu Huria wakiwa katika picha ya Pamoja na Naibu katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana ,utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel alipokuwa akizindua Programu ya mafunzo ya ufundi,mawasiliano na ujuzi wa biashara inayotolewa na chuo kikuu huria ikishirikiana na shirika kutoka Canada linaloitwa Nafasi Opportunity Society(NOS).
Wasichana ambao wapo kwenye Programu ya mafunzo ya ufundi,mawasiliano na ujuzi wa biashara wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Katibu Mkuu na uongozi wa Chuo kikuu huria jana walipokuwa wakizindua program iyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni