Zinazobamba

Baba Levo Afunguka: Trilioni 6.23 za SGR Kigoma, Samia Kuzindua na Diamond, Alikiba Wapange Jukwaani


Mkoa wa Kigoma unajiandaa kushuhudia historia mpya baada ya Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutenga Shilingi trilioni 6.23 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Chipando maarufu Baba Levo, amesema mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa wakazi wa Kigoma na maeneo ya jirani kupitia ongezeko la fursa za ajira, biashara na ukuaji wa uchumi.

Akizungumza na waandishi wa habari Julai 14, 2026, Baba Levo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea mradi huo na kutumia fursa zitakazozaliwa kutokana na uwekezaji huo mkubwa.

Mbunge huyo pia amefichua kuwa uzinduzi rasmi wa mradi wa SGR Tabora–Kigoma unatarajiwa kufanyika Julai 20, 2026, ukiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kivutio kingine cha uzinduzi huo ni burudani kutoka kwa baadhi ya mastaa wakubwa wa muziki nchini. Baba Levo amesema jukwaa litapambwa na wasanii aliowataja kuwa ni "watoto wa Mama", wakiwemo Diamond Platnumz, Alikiba, Chino Kidd pamoja na wengine, huku maelfu ya wananchi wakitarajiwa kujitokeza kushuhudia tukio hilo.

No comments