Zinazobamba

WALIOKOSA AJIRA JESHINI WAPEWA MAJIBU,NI WALE WA WALIOMALIZA MAFUNZO YA JKTSOMA HAPA KUJUA,

Pichani ni Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)  Meja Jenerali Raphael Mehuga picha na maktaba

NA KAROLI VINSENT
JESHI la Kujenga Taifa nchini (JKT) limewataka wananchi kuondoa dhana waliyokuwa nayo, kwamba kila mtu anayejiunga na Mafunzo ya (JKT)  ategemee ajira kutoka katika idara mbalimbali za ulinzi nchini badala yake amesema mafunzo wanayoyatoa yanamanufaa katika kujiari wenyewe.
           Kauli hiyo ya JKT inakuja wiki chache kupita baada ya Vijana waliokuwa kwenye Mafunzo ya jeshi hilo kwa mda wa miaka miwili kuandama huku wakidai kupewa ajira katika idara mbalimbali za ulinzi.
         Akijibu madai hayo leo, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Raphael Mehuga wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa Mtandao huu  Makao makuu ya jeshi la Kujenga Taifa (JKT) yalioko Mgurani Jijini Dar Es Salaam,ambapo amesema anashangaa sana kusikia kuna maandamano ya Vijana waliokuwa kwenye Mafunzo ya JKT,wakidai kupewa ajira huku ikiwa tofauti na Sheria inavyosema.
      “Kiukweli sio kila mtu anayejiunga na JKT apate ajira huku kwetu au maeneo mbalimbali ya ulinzi ndani ya serikali,na mafunzo yetu tunayotoa tunawapa Fursa ya kuweza kujiajiri katika maeneo mengine,ndio maana ukija huku utakuta kila mtu mwenye Kuingia na Fani yake anapewa mafunzo kulingana na Fani yake ili imrahisishie atakapomaliza mafunzo yake aweze kujiajiri”Alisema Meja Mehuga.
       Meja Mehuga aliongeza kuwa hata kablya ya kuanza mafunzo ya watu wanaojiunga na JKT kunakuwa na Fomu Maamlum ambayo mtu anasahini ambapo katika fomu hiyo inasema wazi Dhumuni la kujiunga na JKT kwamba ni kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuongeza ujuzi ili uweze kujiajiri na kuacha kutegemea ajira serikalini.
        Aidha,Meja Mehunga amesema kumekuwa na jitihada kubwa sana zinazofanywa na serikali katika kutoa ajira kwa wale waliomaliza mafunzo ya Kujenga Taifa JKT.

     “Serikali imejitahidi sana katika kutoa ajira kwa wanaomaliza mafunzo ya JKT kwa mfano mwaka huu kunabaadhi ya waliomaliza mafuzo yetu wamepewa mtaji na shirika la nyumba la Taifa wa mashine za kuzarisha matofari,ili iwasaidia katika kujiajiri,”aliongeza

Hakuna maoni