KUPIGWA KWA HAMISI TAMBWE,YANGA YASEMA MAZITO,NI KWENYE MECHI YA RUVU SHOOTING SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Jerry Murro picha na Maktaba |
NA KAROLI
VINSENT
KLABU
ya Soka ya Yanga imelivaa shirikisho la
mpira wa Miguu nchini TFF na kulitaka limwondoe kwenye Ratiba ya mechi
zilizobaki,Mwamuzi aliyechezesha mechi kati yao na Ruvu Shooting iliyofanyika
Jumamosi wiki iliyopita kwa madai mwamuzi huyo ametumwa kwa ajili ya kuihujumu
timu yao.
Na pia Klabu hiyio imesikitika na
ukimya waliokuwanao shirikisho la mpira wa Miguu nchini TFF,katika kuwachukulia
hatua wachezaji wa Ruvu Shooting kwa Fujo walizofanya katika mechi hiyo kwa
Mshambuliaji wake Hamis Tambwe.
Maamuzi hayo yametangazwa leo Jijini
Dar es Salaam na Afisa Habari wa Klabu ya Yanga Jerry Murro wakati wa Mkutano na
Waandishi wa Habari ambapo amesema Klabu hiyo imechoka na hujuma wanazofanyiwa
mwamuzi aliyechezesha mechi yao kwakufumbia makosa aliyoyafanya Beki ya timu ya
Ruvu Shooting kwa kumkaba koo mshambuliaji wao na kumtolea maneno machafu.
“Tunalaani vitendo hivyo na klabu
ya Yanga inasikitika na ukimya
ulionyeshwa na Shirikisho la Mpira TFF,pamoja na Bodi ya Ligi na chama cha Waamuzi nchini FRAT, kwa ukimya na matukio ya kinyama aliofanyiwa mchezaji
wetu Hamisi Tabwe na sisi tunasema hii ni hujuma”
“Viongozi tunalaani vikali
vitendo vya kibaguzi na vya kichochezi alivyoitwa mchezaji wetu kwa kuitwa
Mkimbizi,wakati mchezaji huyo yupo kihalali na sheria ya za mpira wa Mguu
Duniani FIFA ,tunapinga kauli hizi, lakini leo wasimamizi wa mpira wa nchi hii
wako Kimya nasema hatutakubali”alisema Murro.
Murro aliongeza kuwa kwa kuona uvunjifu
huo wa kanuni za mpira amemuagiza mwanasheria wa Klabu ya Yanga kuliandikia
barua Shirikisho la Mpira TFF na
kulitaka kuondoa mara moja jina la mwamuzi huyo wa kati aliyechezesha mechi zao
katika mechi zilizobaki na kutompanga kwenye mechi yeyote inaowahusu Wao,na
endapo TFF wakigeuka basi Klabu hiyo itasusia mechi zote za Ligi kuu.
Kwa upande wake Mshambuliaji wa
Kimataifa kutoka Burundi Hamisi Tambwe aliyefanyiwa Rafu mbaya na Beki ya Ruvu
Shooting alisema anashangaa sana kwa uchezaji mbovu wa wa beki huyo na kusongeza kuwa mchezaji huyo amemtamkia maneno machafu.
“Nasikitika sana kwa mchezaji Yule kuninyanyapaa kiasi hichi kwa kunipiga
hadi kunikaba koo,wakati mchezo mpira ni mchezo wa “Fair Play”sasa nashangaa
kwanini ananifanyia hivi”alihoji Tambwe.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni