Zinazobamba

WANAOMTETEA LOWASSA WAJIBU KASHFA HIZI HAPA,NI HOJA AMBAZO UKAWA BOFYA HAPA KUJUA

Pichani ni Waziri mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa
HIZI NDIZO HOJA 10 ZINAZOMTAFUNA LOWASSA,Soma hapa kujua

Gazeti la Raia Mwema la Novemba 2010 ,
liliripoti na kuonyesha picha ya nyumba
ambayo familia yako inamiliki Uingereza .
Ukasema ni ya mwanao . Je, kwa nchi
maskini kama ya kwetu , ni sahihi kwa
kiongozi mkubwa kumiliki nyumba kubwa na
ya kifahari nje ya nchi ?

2 . Mkapa alipounda Baraza la Mawaziri
jipya mwaka 1995 alikuacha . Wengi
wanasema kwamba Mwalimu alimwambia
asikupe hata Uwaziri je Kwanini mwalimu Alikukataa???

3 . Tangu mwaka 1994 , yaani miaka 20
sasa, Afrika ya Kusini imekuwa inakodisha
nyumba yako Masaki kama Ubalozi wake .
Kuna tetesi kwamba huko nyumba walitaka
kuhama lakini wakaogopa kuihama nyumba
inayomilikiwa na kiongozi mkuu na kuna
tetesi kwamba sasa wanataka kuhama
lakini wanatishiwa kwamba hamuwezi
kuhama nyumba ya Rais ajaye . Ni kiasi
gani cha fedha umepata kwa miaka 20 ya
kukodisha nyumba hiyo ? Je kiasi hicho
kimeripotiwa kwenye fomu ya maadili?

4 . Kuna maelezo kwamba nyumba hiyo ya
Masaki ambayo Mzee Mandela alikuja
mwaka 1994 kuufungua ubalozi mpya wa
Afrika ya Kusini ndicho chanzo kikuu cha
Mwalimu kusema kwamba inakuwaje kijana
wa miaka 41 , akiwa mtumishi ya umma
maisha yake yote na mshahara wake
unajulikana , anamiliki hekalu kama lile na
tena kulikodisha kwa Serikali ya kigeni . Je,
unasemaje kuhusu hili ?

5 . Pia unamiliki ranchi kubwa sana kule
Mzeri Handeni . Ranchi hiyo ilikuwa ranchi
ya taifa lakini ukajimegea na sasa
umeipanua kwa kumega maeneo zaidi .
Ranchi hiyo uliipata ukiwa bado kiongozi wa
umma. Je, mtu aliyewahi kuwa Waziri wa
Mifugo na Waziri Mkuu kujiuzia ranchi
iliyokuwa ya Serikali inaendana na dhana
ya uongozi safi na uliotukuka? Tukikupa
madaraka makubwa zaidi hautajiuzia kila
kitu? Vilevile, katika nchi ambayo wananchi
wengi hawamiliki ardhi , kwa kiongozi
anayetaka kuwa Rais wetu , kuhodhi eneo
kubwa la ardhi , inatuma picha gani kwa
wananchi hao ?


6 . Kwenye sakata la Richmond , ujasiri ni
kusema ukweli au kubwaga manyanga?
Kama ungesema ukweli na usingejiuzulu
kwenye Richmond , Chama kingeathirika vipi
wakati unasema hakuna kosa lililofanyika???

7 . Kwanini kwenye kila tukio la kitaifa
ukisimama tu karibu na Kikwete
unahangaika kutuma picha kwenye
magazeti na mitandao yote ???

8 . Katika miaka yako 40 ya utumishi wa
umma, kuna jipi jipya ambalo umelisahau
na sasa utalifanya kwenye Urais???

9 . Umekuwa Waziri wa Ardhi , mbona
matatizo ya ardhi bado tele nchini ?
Umekuwa Waziri wa Maji , mbona matatizo
ya maji bado tele ? Umekuwa Waziri wa
Mazingira, mbona kuna matatizo ya
uchafuzi wa mazingira ? Umekuwa Waziri
wa Mifugo, mbona wafugaji bado maskini
na wanahangaika ?? huo urais unautaka wa nini kama uwaziri umekushinda???

10 . Kwenye sikukuu hii , kila MNEC kapata
milioni 1 , hizo ni milioni 370 na kila
mjumbe 500 , 000 hizo ni bilioni 2 . Hizi pesa
zinatoka wapi na zitarudishwa vipi? Je,
kuna zoezi la usafishaji wa pesa chafu
linalofanywa kupitia kampeni yako???

Hakuna maoni