Zinazobamba

MAUCHAFU MENGINE BANDARINI HAYA HAPA,PAC YACHACHAMAA-SOAM HAPA


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (Pac), imeagiza Mamlaka ya Bandari (TPA), kurejesha Sh. milioni 62.8 ambazo wamelipana kama posho za safari kwa viwango vipya kabla ya kuidhinishwa na Msajili wa Hazina (TR).

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Zitto Kabwe, akitoa maamuzi ya kamati iliyokutana na uongozi wa TPA na Wizara ya Uchukuzi, kupitia hesabu zao za mwaka 2011/12 pamoja na ukaguzi maalum uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Agizo hilo limekuja baada ya kamati kutaka maelezo ya viwango vipya vya posho ya safari kwa watumishi wa Bandari kwa kudai kuwa wanalipana fedha ya kujikimu nyingi kuliko wabunge.

Kaimu Mkurugenzi wa TPA, Madeni Kipande, alifafanua kuwa malipo hayo baada ya kupendekezwa yaliwasilishwa kwenye Bodi ya Bandari ambao walipitisha na kuanza kulipwa kabla ya kuidhinishwa na TR.

“Tunakiri tulikosea kwenye hilo kwa kuwa malipo yoyote kabla ya kulipwa, ni lazima yaidhinishwe na TR baada ya Bodi kupitishwa, tulilipa viwango vipya bila kupata kibali cha Hazina,” alisema Kipande.

Zitto alisema fedha iliyotumika ni mali ya umma, hivyo ni lazima ikatwe kwenye mishahara ya watumishi wote waliosafiri na kulipwa viwango hivyo kuanzia Januari mwaka huu, kwa kuwa ni fedha ya umma iliyolipwa kinyume cha taratibu na sheria.

“Naagiza fedha zote zilizotumika kwa safari za ndani na nje ya nchi na kutolewa bila ‘approval’ ya TR zirudishwe na tupewa taarifa ya utekelezaji…hamkuwa na sababu ya kukimbilia kulipana fedha hizo bila kuwa na idhini ya TR,” aliagiza Zitto.

Mwenyekiti huyo aliagiza TR kufanya ukaguzi katika taasisi za umma kujua viwango vinavyotakiwa kulipwa kwa watumishi wanaposafiri ndani na nje ya nchi kwa kuwa TPA inaonekana mtumishi wa kawaida anaposafiri analipwa Sh. 123,000 kwa siku huku kiwango kinachojulikana ni Sh. 80,000 kwa siku.

Kwa mujibu wa taarifa ya TPA kwa kamati inaonesha kuwa mfanyakazi wa ngazi za juu anaposafiri ndani ya nchi alitakiwa kulipwa Sh. 270,000 na kwa viwango vipya ni Sh. 500,000 kwa siku, huku mtumishi wa ngazi za chini akilipwa Sh. 320,000

Hakuna maoni