MASIKINI LOWASSA,MIKAKATI YA KUMHUJUMU YAVUJA,SASA APUMULIA MASHINE SOMA HAPA KUJUA
Pichani Ni Edward Lowassa picha na Maktaba |
NA KAROLI VINSENT
MBUNGE wa MONDULI, Edward Ngoyai Lowassa, aweza kuvuliwa
uwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), muda wowote kutoka sasa. Mtandao huu unaripoti.
Hoja ya kumvua
uwanachama Lowassa imepangwa kuwasilishwa katika kikao cha Kamati Kuu (CC),
kinachotarajiwa kufanyika Jumanne wiki hii, mjini Zanzibar.
Taarifa kutoka ndani ya chama hicho
zinasema, mkakati wa kumvua uwanachama Lowassa, unasukwa kwa ustadi mkubwa na
baadhi ya viongozi wandamizi ndani ya CCM ili kumzua kutimiza ndoto yake ya
kuwa rais.
“Ni lazima tumfukuze
uwanachama katika chama chetu. Hakuna namna nyingine ya kukinusuru chama hiki,”
ameeleza kiongozi mmoja mwandamizi ndani ya chama hicho.
Amesema, “Bwana
huyu (Lowassa), amekuwa akikivuruga chama chetu kwa muda mrefu. Tumemvulia,
lakini sasa tumechoka. Nilazima tumuondoe ili kukinusuru chama chetu.”
Ajenda ya
kumfukuza Lowassa kutoka ndani ya chama hicho, imejificha katika kinachoitwa,
“Tathmini hali ya kisasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.”
Lowassa alikuwa
waziri mkuu wa kwanza katika serikali ya Jakaya Kikwete. Anatajwa kuwa miongoni
mwa makumi ya wanachama wa CCM waliotangaza au kutajwa, kusaka urais kwa udi na
uvumba katika uchaguzi mkuu ujao.
Januari mwaka jana, Lowassa na makada wenzake kadhaa walipewa
“onyo” kwa kile kilichoitwa, “kuanza kampeni kabla ya muda kufika.”
Mtoa taarifa wa
Mtandao huu anasema, kabla ya kikao cha CC, kutafanyika kikao cha Kamati Ndogo
ya Maadili na Nidhamu, ambacho kitafanya tathmini ya adhabu zilitolewa kwa
Lowassa na wenzake.
Lowassa
anatuhumiwa kuendelea na mkakati wake wa kampeni kwa kukusanya watu na
kujipanga kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, jambo ambalo viongozi wake wakuu
wanamtuhumu kukipasua chama chao.
Anasema, kikao
cha CC kitatekeleza mradi huo kwa kutumia ripoti zilizotengenezwa na timu za
maofisa usalama wa chama hicho, zilizotumwa mikoa yote ili kukusanya kile
kilichoitwa, “mkakati wa Lowassa wa kusaka urais.”
Kutokana na
hali hiyo, Kamati Kuu iliitaka Kamati ya Maadili kufanya marejeo na kuangalia
utekelezaji wa adhabu kwa makada hao sita.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni