Zinazobamba

MBUNGE WA CCM AMCHAKAZA RAIS KIKWETE,NI KUHUSU WAZIRI MUHONGO,SOMA HAPA

http://mtanzania.co.tz/wp-content/uploads/2014/07/Jakaya-Kikwete1.jpg
Pichani Ni Rais Jakaya kikwete
Mbunge  wa Jimbo la Simanjiro (CCM) Mkoani Manyara,Christopher Ole Sendeka,  amesema endapo  Rais Jakaya Kikwete ,  hatamwajibisha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, atapaleka hoja binafsi bungeni ya kutokuwa na imani viongozi hao.

Sendeka alisema hayo juzi katika mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wachimbaji wadogo na wamiliki wa migodi, uliofanyika  mjini Mererani.
Alisema hoja hiyo anajua itawaumiza na kuwakera baadhi ya watu wakiwamo viongozi wa serikali na CCM, lakini hilo halitamsumbua kichwa bali atapambana kuhakikisha linaungwa mkono kwa asilimia zote.

pichani nMbunge wa Jimbo la Simanjiro (CCM) Mkoani Manyara,Christopher Ole Sendeka


Mbunge huyo aliyekuwa akiongea huku akipigiwa makofi mengi na wachimbaji hao, aliendelea kusema kuwa suala la kupambana na mafisadi linahitaji ujasiri wa hali ya juu kwa kuwa na kichwa kigumu, kwani unaweza kupoteza maisha na yeye yuko tayari kwa hilo.


‘’Kama serikali ikishindwa kumwajibisha Muhongo mpaka Bunge likianza mwisho wa mwezi kuanzia tarehe  27, lazima nipeleke hoja binafsi bungeni kushinikisha hili suala,"alisema.

Alisema viongozi wa ngazi  za juu wa CCM waliwahi kusema kuwa wote waliohusika katika sakata hilo wanatakiwa kuwajibishwa ili kunusuru chama,  lakini mpaka sasa serikali imekaa kimya hakuna kinachoendelea.

Aliwaambia wajumbe kuwa Bunge liliazimia  na kupeleka mapendekezo yake kwa serikali ili waliohusika katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow ya kuchotwa na zaidi ya shilingi bilioni 306, wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na waziri huyo kuondolewa.

Sendeka alisema yeye alisimama kidete kuhakikisha Muhongo anang’olewa katika nafasi hiyo, kwani waziri huyo amekuwa na dharau kwa wawekezaji Watanzania na kusema kuwa hawana fedha za kuwekeza katika sekta ya madini ya gesi.

‘’ Muhongo ni mjeuri na ana dharau   kubwa, ikumbukwe kuwa alisema Watanzania hawana fedha, bali wana pesa  za juisi tu na hawana uwezo wa kuwekeza katika gesi na madini, kwa kauli hiyo tu kiongozi huyo hafai kuwa waziri,’’ alisisitiza.

‘’Sasa kitalu “C “kwa sasa kimechukuliwa na wawekezaji wazawa  ambao tunafahamiana nao na tuna imani watafanya vizuri kama wawekezaji wa nje, ina maana hata hao nao hawana fedha? Ama wana fedha  tu za kutengemneza juisi ?, alihoji Ole Sendeka.

‘’Hii ni dharau kubwa kwa Watanzania wenzangu waliopewa dhamana  ya kuongoza nchi, badala ya kuwasaidia  anawaangamiza,’’alisema.

Kutokana na hali hiyo,  aliiomba serikali kutoacha kutekeleza maazimio ya Bunge, kwani ana uhakika kuwa ataipeleka hoja binafsi mapema mwezi huu, kushinikiza maagizo hayo yatekelezwe.

Akizungumzia uwekezaji, aliwataka wachimbaji na wamiliki wa migodi kuungana na kuwa na mtaji wa kutosha, ili waweze kuwekeza katika sekta nyeti za rasilimali ya nchi kuliko kuwaachia wageni.

Mbunge huyo alisema mitaji midogo waliyonayo wazawa ndiyo kikwazo katika kuwekeza sekta ya gesi na madini, hivyo aliwataka kuungana ili kupata fursa hiyo kwa maslahi ya nchi.

Pia alitoa wito kwa wachimbaji hao na wamiliki wa migodi kumuunga mkono mwekezaji mzawa aliyechukua kitalu C na kusema kuwa hiyo imemfurahisha yeye binafsi na kusema kuwa kero zilizokuwa awali zitapata ufumbuzi kwa pande zote kukaa meza moja

Hakuna maoni