HABARI KUBWA-MAUAJI YA MAALBINO YAWAPONZA WAGANGA,WAZIRI CHIKAWE AAPA KUFA NAO SOMA HAPA KUJUA
Pichani ni Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini dar |
NA KAROLI
VINSENT
WAZIRI wa
mambo ya ndani ya nchi Mathias Chikawe kwa kushirikiana na Mkuu wa jeshi la
Polisi nchini IGP Ernest Mangu wamewataka
waganga wa kienyeji wanaofanya
shughuli za kupiga Ramli kuacha maramoja kufanya kazi hizo,kwakuwa wamekuwa
wakihusika na vitendo ya mauaji wa watu wenye Ulemavu wa ngozi Maalbino.
Na pia Jeshi hilo limeanzisha msako
nchi nzima na kuwasaka popote walipo watu
wanaohusika na vitendo vya mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi Albino ili sheria ichukue mkondo wake.
Waziri Chikawe ameyasema leo Jijini Dar
es Salaam wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari,ambapo amesema nia ya
serikali ya kupiga marufuku waganga wa
kienyeji wanaofanya kazi ya kupiga ramli unalenga kukomesha vitendo vya mauaji wa
maalbino kutokana na waganga hao wa kienyeji kuhusika kwa kiasi kikubwa katika
maauaji hayo
“Jeshi la polisi litafanya operesheni
maalum ya kuwatafuta wauaji wa maalbino na waganga wanaopiga ramli na tutashirikiana
na wadau mbalimbali ili kuwabaini waganga wa kienyeji wanaofanya kazi ya
upigaji ramli na kuwachukulia hatua kali ili kukomesha vitendo hivi na
tukiwakamata tutawachukulia hatua kali za kisheria”alisema Waziri Chikawe.
pichani wa kwaza kulia ni Igp Ernest mangu akiwamakini |
Waziri Chikawe aliongeza kuwa Jeshi
hilo la polisi litashirikiana na wizara ya TAMISEMI ambao wanahusika na kusimamia
serikali za mitaa ili kuwabaini waganga hao wanaopiga ramli.
“Nawahakikishia
wananchi tutawapata walipo wanaofanya vitendo vya upigaji ramli ambao tunajua
tukishirikiana na Tamisemi ambao ndio wanasimamia serikali za mtaa kwakuwa wako
maeneo yao wanaokaa kwani viongozi wakijiji watatusaidia kuwapata”
Alibainisha kuwa watu wanaozania serikali
itashindwa kuwapata waganga hao basi wanajidanya kwani serikali imejipanga na
kutomeza vitendo vya mauaji ya Maalbino kama ilivyoweza kupoteza vitendo vya
umwagi wa watu tindikali.
Mwenyekiti wa chama cha Maalbino Ernest Kaiwa akufafanua jambo |
Kwa upande
wake Mwenyekiti wa Chama cha Maalbino nchini
Ernest kaiwa aliishukuru jeshi la polisi nchini kwa opareshen walioianzisha
na kusema itawasaidia kuondoa hofu
waliokuwa nayo sasa kuhusu maisha yao.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni