Zinazobamba

CHAMA CHA ACT WAFANYA UASI MWENGINE,WAGEUKANA WENYEWE KWA WENYE SOMA HAPA

Turn off for: Swahili
Alliance for Change and Transparency
(ACT-Tanzania)
___________________________
________

Maazimio ya Halmashauri Kuu ya ACT-Tanzania kufuatia Mkutano wake wa Pili Uliofanyika  Jumatatu Tarehe 12 Januari 2015 katika Hoteli ya Kagame, Jijini Dar es Salaam

Halmashauri Kuu ya ACT-Tanzania ilifanya Mkutano wake wa Pili wa kawaida siku ya Jumatatu tarehe 12 Januari 2015 katika Hoteli ya Kagame Jijini Dar es Salaam. Pamoja na mambo mengine, Halmashauri Kuu ilipokea na kujadili taarifa mbalimbali na kutoa maamuzi na maazimio katika mambo mbalimbali kama ifuatavyo:
1.      Halmashauri Kuu ilipokea, kujadili na KUPITISHA k Mwongozo na Kanuni za Uchaguzi ndani ya Chama cha ACT-Tanzania. Halmashauri Kuu imepanga uchaguzi ndani ya chama ufanyike kuanzia tarehe 17 Januari 2015 katika ngazi ya Shina na kukamilika tarehe 28 Machi 2015 katika 
ngazi ya Taifa.
Kadawi limbu
2.      Halmashauri Kuu ilipokea na kujadili Taarifa ya Kamati Maalumu ya Nidhamu iliyoundwa na Kamati Kuu kuchunguza masuala ya nidhamu ya viongozi wa Kitaifa, ambao ni Mwenyekiti wa Muda wa Taifa Ndugu Kadawi Lucas Limbu na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Leopold Mahona. Baada ya mjadala wa kina na kuridhishwa na makosa yaliyotendwa na viongozi hawa, Halmashauri Kuu imetoa maamuzi yafuatayo:
a.       Imemsimamisha Ndugu Kadawi Lucas Limbu katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Muda wa Taifa baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wajumbe 57 (87.7%) kati ya wajumbe 65 waliohudhuriwa.
b.      Imemwondoa katika nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu Ndugu Leopold Mahona baada ya wajumbe 57 (87.7%) kupiga kura za kuunga mkono pendekezo hilo kati ya wajumbe 65 waliohudhuria.
3.      Halmashauri Kuu imeazimia kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na imeagiza Kamati Kuu kujiandaa na uchaguzi huo katika ngazi zote.

Pamoja na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania


Samson Mwigamba

Katibu Mkuu ACT-Tanzania.

Hakuna maoni