MTANGAZAJI ZEMBWELA APATA SHAVU KUBWA KUWAI PATA MAISHANI MWAKE SOMA HAPA
Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(katikati)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa Promosheni mpya inayojulikana kama JayMillions itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku.Kushoto ni Balozi wa promosheni hiyo Hilary Daud”Zembwela” na kulia ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Balozi wa promosheni ya JayMilions Hilary Daud ”Zembwela” (kushoto) akionesha bango linaloelezea jinsi ya mteja kujua kama ameshinda katika Promosheni hiyo iliyozinduliwa na Vodacom Tanzania leo itakayowawezesha wateja wa kampuni hiyo kujishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 30/- Ili kujua kama umeshinda mteja anatakiwa kutuma SMS moja tu kila siku yenye neno “JAY” kwenda namba 15544.Wengine kutoka kulia Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo Kelvin Twissa.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Vodacom imezindua promosheni kubwa kuliko zote katika historia ya michezo ya bahati nasibu nchini Tanzania ambapo wateja watajishindia pesa taslimu Sh. bilioni 30/- katika zawadi ndani ya kipindi cha siku 100.
Akizungumza na waandishi wa habari jjijini leo ,Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania Rene Meza amesema promosheni hii inajulikana kama JayMillions na inawahusisha wateja wote wa Vodacom na ni ya kwanza ya aina yake kwani, “kiasi kikubwa cha fedha kitatolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”
Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/- na washindi mia moja wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia washindi elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh. 1000/- kila siku.
Meza ameongeza kuwa hii inadhihirisha dhamira ya kampuni ambayo mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wake pia ina dhamira ya kubadilisha maisha ya wateja kuwa murua zaidi “ambao wamekuwa wakiendelea kujiunga na familia ya Vodacom kila siku.”
Kwa upande wake, Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Vodacom, Kelvin Twissa amesema ili kushiriki katika promosheni hii, mteja yeyote wa Vodacom, aliyeko popote nchini anahitaji kutuma SMS moja tu yenye neno “JAY” kwenda namba 15544 kila siku ili kujua kama ameshinda au la. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata. Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu.
“”Tofauti na promosheni zilizopita, JayMillions ni rahisi sana kushiriki. Tuma ujumbe mfupi mmoja tu na mara moja tu kila siku. Hakuna maswali mengi, wala chemsha bongo na hivyo kufanya hii kuwa promosheni inayotoa nafasi kwa wateja wengi kuibuka washindi. Cha muhimu ni kuhakikisha kila siku unatuma ujumbe mfupi,” alieleza Twissa.
Alisema kila siku namba zilizoshinda zitapatikana kupitia mfumo mahsusi wa promosheni hii. “Ili kujua kama namba ya mteja imechaguliwa, tunapenda kukusisitizia mteja wetu kutuma ujumbe mfupi wa “JAY” kila siku kwenda 15544 ili wasipoteze bahati zao iwapo namba zao zitakuwa zimechaguliwa. Bila kufanya hivyo, wanaweza kupoteza mamilioni kwani hawatoweza kujua kama namba zao zilichaguliwa kama washindi ambapo zinachaguliwa kila siku,” alisisitiza Twissa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni