Zinazobamba

WAFANYA BIASHARA MACHINGA COMPLEX WAMVAA MUSA ZUNGU, WASEMA HOJA YAKE BINAFSI IMELENGA CHUKI DHIDI YA MKURUGENZI

Kaimu mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la machinga Complex Bw. Gerald Mpagama akifafanua jambo mbele ya Mtandao huu kuhusiana na kulaani vikali hoja binafsi iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo La Ilala , Mh.Musa Zungu kule Bungeni, Zungu alinukuliwa Bungeni akisema kuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dreslaam, MH. Kabwe anachangia kuwafanya wafanyabiashara wadogowadogo kufanya vurugu kutokana na uongozi wake mbovu.

Wafanyabiashara wa soko la Machinga Complex wameibuka na kulaani hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni N a mbunge wa Jimbo hilo, Ndg. Musa Zungu na kusema kuwa hoja hiyo imelenga kuwafanya wafanya biashra wa soko hilo kuendelea kuwa masikini huku yeye akifaidika na maslahi yake mwenyewe,
Akizungumza na Mtandao huu mapema hii leo, Kaimu mwenyekiti wa Soko hilo Ndg. Gerald Mpagama amesema wafanyabiashara wa soko hilo wanalaani hoja hiyo,
SISI wafanyabishara wa soko hili la Machinga complex tunalaani vikali hoja binafsi iliyotolewa na mbunge wetu kuwa eti Mkurugenzi wa jiji hili la Daresalaam akisaidiana na Mkuu wa mkoa huu  wanashiriki kusababisha vurugu za wamachinga bila sababu za msingi na kusema kuwa hoja hiyo imelenga kumjenga yeye kisiasa huku wafanyabishara wakiumia,
Ameendelea kusema kuwa kama kweli Zungu alikuwa na uchungu na wafanyabiashara, kwa nini asingewashirikisha  katika kupeleka hoja hiyo, na badala yake tunaona ameibuka kutoka kusikofahamika nakuibua hoja ambayo ni kandamizi kwa walala hoi wa soko la machinga complex,
Kwa kweli Zungu ametusikitisha sana, hata kama ndiyo utawala lakini hakuna utawala wa mabavu kama anavyofanya ayeye, Tunafahamu serikali ya JK ni sikivu na ndio maana akaletwa mkurugenzi ambaye anaijua kazi yake vizuri lakini watu wachache wanalenga kumuangusha, aliongeza Bwana Mpagama.


Mpagama akifafanua kwa hisia kali, wamesema hataka kama anajiandaa kwa uchaguzi basi atende kazi zake kwa weredi ili hata akiondoka watu waweze kumkumbuka kwa wema wake kuliko kucha matatizo ambayo yatachafua jinalake.



Hakuna maoni