|
Kaimu
mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya hali ya hewa Eng. James Ngereja
akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari katika mkutano
uliowakutanisha wanasayansi wa vyuo vikuu mapema hivi karibuni, Eng.
Ngeleja amesema ripoi ambayo imezinduliwa inaweka wazi namna ya Tabia
nchi ilivyo kwa sasa |
Mamlka ya hali ya hewa hapa nchini TMA imewataka wakuu wa vyuo kuhakikisha kuwa wanafunzi wao wanahamasishwa kufanya tafiti za Tabia nchi ili tafiti hizo ziweze kulisaidia taifa hususani katika kipindi hiki ambacho taifa linahitaji taarifa muhimu kuhusu Ttabia nchi,
Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti ya Tano inayohusu Mabadiliko ya Tabia nchi ambayo hufanywa kila baada ya mwaka mmoja na nusu, Mkurugenzi mtendaji wa malka hiyo , Bi. Agness Kijazi amesema ni wakati sasa wanafunzi wetu wakafanya tafiti za kuliletea taifa tija.
Kijaiz ameongeza kusema kuwa Taifa la Tanzania linahitaji taarifa hususani hizi za tabia nchi ili kwenda sambamba na mahitaji ya mamlaka ya hali ya hewa duniani ambayo inahitaji kila taifa duniani lihakikishe linakidhi vigezo walivyojiwekea hadi kufikia mwaka 2016.
|
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa Dk Agness Kijazi akifafanua jambo katika mkutano huo wa siku moja uliowakutanisha wanataaluma wa kisayansi kujadili lipoti ya tano inayohusu hali ya hewa, Kijazi ametumia fursa hiyo kuwataka wakuu wa vyuo hapa nchini kuwataka wanafunzi wao kufanya tafiti za Tabia nchi kwani kwa sasa Taifa linahitaji taarifa hizo ili kutejkeleza vizuri mpango wa mamlaka ya hali ya hewa Duniani |
|
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya hali ya hewa hapa nchini, Bi. Agness Kijazi akiwa katika picha ya pamoja na wadau kutoka katika vyuo vikuu hapa nchini, Wanafunzi hasa wa sayansi ni wakati wao sasa kuhakikisha wanatumia fursa hii ili kufanya tafiti zitakazo leta tija kwa taifa. |
wanazindua ripoti ya tano utafiti wa tabia nchi, walikutana na wanasayansi wa vyuo vikuu nchini, kubwa
Hakuna maoni
Chapisha Maoni