SIRI ZAANZA KUFICHUKA JUU YA KIGOGO WA IPTL,NI JAMES RUGIMALIRA,TOKA BIASHARA YA MCHELE HADI KUFUA UMEME SOMA HAPA KUJUA
pichani ni Kushoto ni Bwana James Rugimalira ambaye ndio kigogo wa IPTL picha na maktaba |
Baada ya kuwa kwenye mgogoro wa umeme nchini Tanzani a yapata miaka karibu 15 sasa, Chanzo chetu kikaamua kufuatilia hasa tatizo lilianzia wapi na nani waliohusika.
Chanzo hicho kilianzia
ndani ya Wizara ya nishati na madini kwa kufuatilia mikataba iliyoyaingiza
nchini makapuni ya uzalishaji umeme,
Taarifa halisi na nyaraka zinabainisha
kuwa tatizo hili lilianza baada ya mfanyabiashara maarufu bwana James Rugemalira
kuiingiza nchini kampuni ya IPTL kutoka Vietnam!
Mchakato unatajwa kuwa ndugu James
Rugemalira alikuwa akifanya biashara ya Mchele kutoka Vietnam mwaka 1995,
katika harakati zake za kibiashara huko Vietnam aliweza kuunda urafiki na
wanaotajwa kuwa wamiliki wa IPTL hii ya sasa.
Mwaka 1997 kulianza kutokea uhaba wa umeme
Tanzania ambapo ndani ya Wizara ya nishati na Madini kulipendekezwa itafutwe
kampuni itakayozalisha umeme wa dharula wa haraka zaidi ili kunusuru taifa:
Kamishna wake alikuwa ni Ndugu Patrick
Rutabanzibwa ambae katika uchunguzi umebaini ni ndugu na James Rugemalira ambae
ni mfanyabiashara na mmiliki wa Mabibo Heineken ya Ubongo,
Baada ya Rutabanzibwa kuona kuwa pale
wizarani kuna mwanya wa kupiga hela aliweza kuongea na mdogo wake ambae katika
nyaraka nyingi anatajwa zaidi kwajina moja tu la Rugemalira kuwa atafute
kampuni ya kufanya kazi hiyo haraka sana!
Rugemalira bila kusita akawashtua
washikaji zake ambao taarifa kutoka Vietnam zinasema waliokuja si wale waliokuwa
na urafiki na Rugemalira bali ni marafiki wa marafiki wa Rugemalira kutoka
Malaysia.
Na hawakuwa na sifa ya kiushawishi ya
kufanya mradi wa kimataifa ingawa waliweza kushirikiana pamoja bila tatizo
kwakuwa yalikuwa ndio malengo yao ya pamoja!
Makubaliano ya mkataba ilikuwa ni
mashine zitakazoletwa na IPTL, zitakuwa na mfumo wa kutumia gesi na mafuta,
hilo liliingizwa katika makubaliano ya mkabata kwakuwa tayari kulikikuwa na
mradi wa songas uliokuwa ukiendelea kujengwa .
Katika uchunguzi ulioenda
sambamba na mahojiano ya kijasusi, bwana Rutabanzibwa anasema miezi miwili
baada ya kusaini mkataba ule alishangazwa kubaini kuwa IPTL inaleta mitambo
inayotumia mafuta tu na alipouliza wasaidizi wake wakamuambia mkataba
unasemaje? Akaamua kwenda kuangalia upya mikataba aliyohusika na yeye kuisaini
lakini anasema "nilishangaa kuona kipengele kilichokuwa kikisema kuwa
genereta hizo zitakuwa na uwezo wa kutumia gesi kimetolewa" nakuwa
generata za mafuta mazito tu.
Baada ya kupandishwa nakuwa
Katibu mkuu, anasema "nilizuia kuletwa kwa mitambo hiyo kwakuwa
nilizungukwa na kubadilishiwa mkataba feki"
Uchunguzi umebaini Bwana Rutabanzibwa
hakuzuia ama lengu la kuzuia halikutimilika na alihongwa!
Ukweli unabainika katika
dokezo la 12/6/2001 toka kwa kwa kigogo mmoja wa juu wa sasa jina tunalo ilikiwa limeandikwa kwa mkono na kalamu ya
wino mwekundu "Kama nilivyokuahidi jana katika kikao chetu, waambie
wailete hiyo mitambo kama ilivyo na mimi nitafanya kama tulivyokubaliana"
chini ikasainiwa Jina la kigogo huyo wa juu hapa nchini jina limehifadhiwa
Licha ya hivyo bado
uchunguzi unazidi kubaini ushirika wa karibu wa Kigogo huyo wa juu hapa nchini
jina linahifadhiwa na mtu anaetajwa kuwa ni Rugemalila anaeonekana alikuwa na
nguvu ya ushawishi kwa Rutatabanzibwa na wavietnam wa IPTL.
Kwakuwa baada ya kufuatilia kwa kina
imegundulika kuwa katika account ya bank (CRDB) ya biashara ya mchele ya
Rugemalila, kila mwezi kiasi cha pesa Shilingi milioni 130 kilikuwa
kikihamishwa kwenda kwenye account mbili tofauti lakini za mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina Asha Salum Mohamed mkazi wa Arusha mjini,
Jambo la kuvutia zaidi nikuwa pesa hizo
zikifika kwenye hizo account zilikuwa zikitolewa ndani ya masaa 48, na
kuingizwa kwenye akaunti ya ya Abas Zuberi Musa (NMB) na hapo hutolewa siku
hiyohiyo (Cash) na kupelekwa mojakwa moja katika akaunti ya siri ya kigogo mmoja jina tunalo iliyopo Standard Chartered Bank,
Abas Z. Musa kwa sasa ni
mmoja watu ambao wako katika idara moja ya ulinzi hapa nchini tena akitumika
sana kwa mambo binafsi ya Kigogo huyo wa Juu hapa nchini!
Huo ndio ushikiano wa wa
Kigogo huyo na james Rugemalira katika biashara ya mchele,
Bado Chanzo chetu kinaendelea
kufuatilia kwa undani kujua mambo makuu mawili kwanza:
(1) Kwanini aliamua kufanya
biashara hiyo ya mchele kwa siri na kuchukua faida kwa siri kubwa hivyo?
(2) Iwapo Kigogo huyo wa
Juu hapa nchini alihusika moja kwa moja au kwa aina yoyote ya biashara ya IPTL
Chanzo hicho kitafanya
uchunguzu huu kwa undani na kujua nini hasa kipo kwenye tatizo la umeme
Tanzania, kwa sahv kinaanza na IPTL kisha wengine watafuata!
Kwasababu
za kiuchunguzi nyaraka sitaziweka hapa mpaka uchunguzi ukamilike wote!
Uchunguzi: Chanzo cha
matatizo katika sekta ya Umeme Tanzania na ujio wa IPTL
Page 3 of 3 First 123
Jason Bourne 21:41 23rd
June 2012
Hakuna maoni
Chapisha Maoni